Ku'mbrand msanii wa kibongo na kufanikwa

theHAVARD_product

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
289
Reaction score
192
Kuna Wasanii nimekaa chini na kufikiri labda wanakosa Management nzuri ndio maana labda hawa'shine sasa. Ila ni Wazuri kiukweli,wanaweza ,wanajua nk.
Wasanii wa Bongo wengi bila Management nzuri kusurvive ni kazi na sio Tanzania tu na hata huko duniani. Bila kuwa na Record deal nzuri na Management nzuri ni ngumuu mnooo.

Kama si kuonekana na Usher Raymond wengi tusingemfahamu hata kumtambua Justin Bieber'JB':smiling: pia Nick Minaj ni matokeo ya Lil' Wayne na Cash Money Records nk.

Management ni kila kitu kwa Msanii.

JE,KUMBRAND MSANII INACHUKUA MUDA GANI?

Mimi nafikiri miezi sita tu inatosha kumbrand Msanii. Mfano,Sarah Kaisi aka SHAA chini ya New 'BRANDING MANAGEMENT' ya Mkubwa na Wanawe kwa kushirikiana na Babu Tale. Ameanza kuvuma na kueleweka Uswahilini kwa kipindi kifupi tu baada ya kutoa wimbo wa SUGUA GAGA. Amefanikiwa pia YouTube baada ya wimbo huu.

GHARAMA ZA KU'MBRAND MSANII.

Kulikuwa na Ugomvi kati ya B'HITZ MUSIC GROUP na Msanii Mabeste kuhusu gharama walizotumia Ku'mbrand. Wenyewe B'HITZ walikuwa wanasema wametumia zaidi ya TSH Millioni 20 tangu waanze kuM'manage nafikiri ulikuwa Uongo wa Mchana KWEUPEE. Sidhani kama Ilizidi hata TSH Millioni 8 katika KuM'Brand Mabeste!!

Kwa Uzoefu wangu Msanii mwenye Jina kama PASHA,TIMBULO anaweza Kugharimu 'NEW BRANDING' ya kama TSH Millioni 15 na akafanikiwa vizuri sana.

JE,WASANII WAKO TAYARI?!

Sidhani kama hakuna Msanii asiyetaka Kufanikiwa kama Diamond Platnumz,Amekuwa mfano amekuwa Dira kwa Wenzake! Kila mtu sasa anataka Ku'drive gari nzuri,Kujenga Nyumba,Kumiliki Assets zake,Kusafi Ulaya Bila kusahau kuvaa vizuri.
Wamejifunza makosa kutoka kwa kina Mr.NICE na wengineo.

WASANII AMBAO NAHISI WAMEKOSA 'BRANDING'.


  1. PASHA- Ni Msanii mkali sana . Tangu Namfahamu miaka ya 2007,anachokosa ni Management tu.
  2. TIMBULO- Anajitahidi sana. Anahitaji Nguvu ya kuJipanua kimataifa.

Wengine nitawaongeza.

JE,INALIPA KU'MBRAND MSANII?!

Inalipa,Muhimu ni Kuweka Mkataba na Kutafuta Msanii mzuri.
Nadhani Managemnet ya SNURA itakuwa inachekelea sana Pesa baada tu ya Nyimbo Mbili. Ameweza kuzunguka karibu Tanzania Nzima na Baadhi ya Nchi za Ughaibuni.

Maoni,MUHIMU!
 
Menina anahitaji management tu...atatoka hata zaidi ya Diamond na akijua style gani atumie
 
Menina anahitaji management tu...atatoka hata zaidi ya Diamond na akijua style gani atumie
Nimemuona katika Shaghalabhagala amekuja na Idea nzuri,Obvious ametumia ufundi sana kulitumia hili neno. Anahitaji Management wigo wake hasa mtaani,Wimbo ni mzuri lakini haujafika mtaani sana. Na kwenye socia sites pia.
 
Tatizo kubwa ya wasanii wa bongo ni kutojitambua thamani walionayo kama brand.Pili wanashindwa mbinu za wao kudumu kwa muda mrefu katika soko la muziki i.e sustainability.Pia wanakosa management nzuri yenye upeo wa muziki na inayo wajali.Ma manager wengi wa wasanii wa bongo hawana connection nyingi na wadau wengi wa muziki wa kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…