Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,414
- 3,118
Kama ilivyo binadamu hatuja kamilika basi tukumbuke kutokuwa na neno KAMWE or Never, hivyo lazima siku zote uwe na Asilimia moja ya kutokwenda unavyotaka kwa Jambo lolote lile.
Hii itakusaidia kufanya maamuzi sahihi pale mambo yanapokwenda vile usivyo taarajia mfano:
Lazima uwe na 1% kwamba mkeo/mmeo au mpenzi ni binadamu hivyo anaweza cheat au kukosea sana, siku ukikuta imetokea hii 1% itakusaidia utarelax na kufanya maamuzi sahihi yenye faida kwako.Hii itakusaidia kufanya maamuzi sahihi pale mambo yanapokwenda vile usivyo taarajia mfano:
Lazima uwe na 1% kwamba biashara unayofanya kuna uwezekano ikaja ikakwama, ukaibiwa au dhurumiwa au filisika au ikapitia Changamoto kubwa, hii 1% itakusaidia yakitokea hutafanya maamuzi mabaya.
Unakwenda kusoma, lazima uwe na 1% kuna kufeli hata kurudi nyumbani.
Unamwamini rafiki au ndugu lazima uwe 1% kwamba yeye ni binadamu lolote linaweza tokea.
Utagombea Uongozi lazima uwe 1% kwamba kunakushindwa hata kama kuna magoli ya mikono yanategemewa
Mambo ya LAZIMA au HAIWEZEKANI. Matokeo yake huwa sio mazuri sana.
Hivyo kwa kifupi 1% au Asilimia moja ni muhimu kuwa nayo ili uweze kufanya maamuzi sahihi hasa pale una patwa na hasira sana, huzuni sana au hali ya kukatiswa sana tamaa.