Kumbukizi: Julai 2017 Rais Hayati Magufuli aliokota vichwa vya treni bandarini

Kumbukizi: Julai 2017 Rais Hayati Magufuli aliokota vichwa vya treni bandarini

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Nawakumbusha tu jamani kuwa mwaka 2017 RAIS shupavu na mtetezi wa wanyonge aliokota vichwa vya treni bandarini.

Hii nchi imepitia misukosuko kuliko nchi zote duniani.

24fb2aec-acf2-407c-b9a6-37db48680cb2.jpg
 
Tuwekee sawa taarifa yako! Aliokota kwa namna gani? TRL ambao ndiyo wenye shirika havikuwa vyao ama? Au kuna mtu binafsi aliingiza hivyo vichwa ila hakutaka kujitokeza?
 
Nawakumbusha tu jamani kuwa mwaka 2017 RAIS shupavu na mtetezi wa wanyonge aliokota vichwa vya treni bandarini.
Hii nchi imepitia misukosuko kuliko nchi zote duniani.
View attachment 2483828
IMG_20230116_200853.jpg

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko aliweka bayana kwamba vichwa hivyo vina nembo ya TRL na kwamba ulitokea mgogoro kati ya shirika hilo na kampuni iliyotengeneza vichwa hivyo baada ya kubainika kuwa mchakato wake wa ununuzi haukuwa sahihi.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba ununuzi huo umegharimu Sh70.5 bilioni ambazo zote zilishalipwa. “Mradi huu wa ununuzi wa vichwa 13 vipya vya treni ni sehemu tu ya mpango kabambe wa Serikali wa kuifufua na kuiimarisha TRL chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuhusu vichwa hivyo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani amesema wizara haikuwa na taarifa juu ya ujio wake na kwamba taarifa ya Rais ni sahihi.

Ngonyani amesema wizara imeziagiza TRA na TPA kuandaa taarifa kuhusu vichwa hivyo vilivyoshushwa bandarini bila wamiliki wake kutambulika na pia wameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi juu ya suala hilo.
 
Back
Top Bottom