Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,962
- 7,830
Tarehe kama ya leo miaka 21 iliyopita Dunia ilimpoteza kiungo mahiri wa Man City na timu ya Taifa ya Cameroun, Marc-Vivien Foe.
Foe alidondoka uwanjani dakika ya 72 wakati wa mchezo wa Kombe la Mabara, kati ya Cameorun dhidi ya Colombia katika hatia ya nusu fainali ambapo michuano hiyo ilikuwa inafanyika Ufaransa.
Wakati Foe anadondoka hakuwa na mtu karibu yake alikuwa mwenyewe katikati ya uwanja. Chanzo ilikiwa ni tatizo la moyo. Watu wa matibabu waliingia uwanjani na kutumia karibia dakika 45 kujaribu kuokoa uhai wake lakini ikashindikana. Akapoteza maisha.
Kwa heshima ya Foe, Klabu ya Manchester City aliyokuwa Foe anacheza kwa mkopo, ikastaafisha jezi namba 23 na haitumiki tena klabuni hapo.
Marc-Vivien Foe akazikwa kitaifa huko kwao Cameroun katika mazishi ya kitaifa yaliyoandaliwa na serikali.
Marc-Vivien Foe ni miongoni mwa mashujaa kule kwao Cameroun.