Karibu miaka 20 kasoro sikuchacke, tangu afariki, kumbukumbu za TX Moshi William bado zinaishi kwa mashabiki wa muziki wa dansi. Umaarufu wake ulijengwa na tungo zenye maudhui yenye mafunzo kwa jamii, zilizompa heshima kubwa katika maisha yake ya muziki.
Alizaliwa mwaka 1958 Korogwe, Tanga kwa jina la Shaban Ally Mhoja Kishiwa, baadaye baadae akajulikana kama Moshi William. Safari yake ya muziki ilimpitisha katika bendi kama Polisi Jazz kabla ya kujiunga na Juwata mwaka 1982, na baadaye kung’ara zaidi akiwa ndani ya Msondo Ngoma Music Band.
Mwaka 2005 alipata ajali ya gari eneo la Mivinjeni, barabara ya Kilwa, iliyomvunja mguu. Mwaka 2006 alianza matibabu Kibaha, baadaye akahamishiwa Hospitali ya Regency na hatimaye Muhimbili National Hospital, ambako alifariki dunia Machi 29, 2006. Kwa mujibu wa mjane wake, Bi Asha Seif, chanzo cha kifo kilihusishwa na matatizo ya mguu pamoja na figo. Alizikwa Keko Machungwa, Dar es Salaam.
Katika muziki, aliacha hazina ya nyimbo nyingi zenye mafundisho kama Ashibae, Mwaka wa Watoto, Msafiri Kakiri, Asha Mwanaseif, Kaza Moyo, Ajuza, Ndoa Ndoano, Ajali, Isihaka Kibene, Harusi ya Kibene, Piga ua Talaka Utatoa na nyingine nyingi, akiwa amerekodi takriban albamu 13. Wimbo Ajali baada ya Kupata ajalil.
Ubora wake ulimfanya kulinganishwa na Madilu System kutokana na mtindo wa uvaaji, nywele na uimbaji. Pia alitunukiwa tuzo mbalimbali za muziki zikiwemo Kilimanjaro Music Awards.
Jina TX alipewa na Julius Nyaisanga kutokana na ubora wa tungo zake. Licha ya mafanikio, maisha yake ya utotoni hayakuwa tulivu—aliwahi kusema migogoro ya wazazi wake ilimfanya kuishi kwa kuhama-hama na kulelewa na baba wa kambo kwa muda mrefu.
Ndani ya Msondo, alifanya kazi na wanamuziki waliotangulia mbele ya haki kama Suleiman Mbwembwe na wengine wengi. Mbwembwe alikuwa na sauti ya kipekee na mara nyingi waliimba kwa kupokezana. Kupotea kwa majina haya kumeacha pengo kubwa, na kwa mujibu wa Waziri Dewa, ni vigumu kumpata mrithi wa sauti na mvuto kama wake.
Aliacha mjane na watoto watano Hassan, Maika, Ramadhani na Maada (wa mama mmoja), pamoja na mwingine ambaye jina lake halikufahamika. Hassan aljaribu kufuata nyayo zake jukwaani, lakini hakufikia kiwango chake kwa mujibu wa mashabiki.
Kisanii, TX Moshi alikuwa mbunifu mkubwa aliebuni mitindo kama mambo hadharani na chombezo, akitumia vionjo kama “we nani”, “kidogo ltu”, “kwanini lakini”, “watoto wanachezea umeme”, “discipline”, “fair play” na vingine vilivyoongeza ladha ya nyimbo zake.
FADHALI MODI MNAWEZA HAKIKISHA TAARIFA VIZURI, NA WADAU WENGINE KAMA KUNA MAHAKI HAKUKO SAHIHI ILI KUWEKA JUMBUKUMBU VIZURI.
JE WEWE UNAMKUMBUKA TX MOSHI KIVIPI KATIKA ULIMWENGU WS DANCE