Wakuu,
Tunapoelekea ukingoni mwa mwaka 2025, kuna nyimbo ambazo zikipigwa, moyo lazima usimame na kutafakari. Moja ya nyimbo hizo ni ule wimbo maarufu wa miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 uitwao
"Ni Nani".
Swali kuu la wimbo huu linabaki kuwa alama ya vizazi:
"Ni nani anayeweza kusema amemaliza mwaka salama kwa nguvu zake yeye mwenyewe?"
Hii ilikuwa ni kazi ya kishujaa kutoka kwa
Kwaya Kuu ya Patandi (Patandi Teachers' College Choir -KKKT). Ingawa wimbo huu uliandaliwa kuanzia miaka ya 90 (katika albamu ya
Msifungiwe Nira), toleo hili la video tunaloliona lilipata baraka za kisheria na usajili mnamo mwaka
2001 (© 2001) kupitia ushirikiano mkubwa wa kikanda.
Waliofanya Maajabu Haya (Kikosi Kazi)
Hatuwezi kuutaja wimbo huu bila kuwataja mashujaa waliosimama mstari wa mbele kuhakikisha ujumbe huu unatufikia kama unawafahamu na Bado wapo hai wasalimie Mimi namfahamu Lukas Kariongi ambaye alikuwa Ni Sound na photography:
- Uongozi Shupavu: Chini ya Mwenyekiti Mica Mwinyimali, Katibu Elituliza Joel Pallangyo, na Mtunza Hazina Ndelilio E. Sumari.
- Mwalimu wa Kwaya: Fundi wa sauti na uongozi wa kiufundi, Moses Sululu, akisaidiwa na Mtunza Nidhamu Jackob Benjamin.
- Walezi: Waliosimama kama nguzo ya kiroho, Elishilia D. Kaaya na Aishiel Sumari.
Safu ya Waimbaji (Sauti za Dhahabu)
Amon Mfiome, Lilian F. Swali, Lucy S. Mbise, Godson Pallangyo, Prisca E. Sikawa, Beatrice T. Kaaya, Magdalena Elibariki, Light W. Pallangyo, Naomi N. Isangya, Lucy Shirima, Ana E. Mrema, Estomih J. Sumari, Mathias J. Sumari, Elibariki Munuo, Clemence J. Sumari, Dausen W. Pallangyo, Nehemiah L. Kaaya, Eddie Mpelasoka, Neema William, Rose William, Jackline Swai, Mary Laban, Vero John.
Mapinduzi ya Production: Simanjiro na Lushoto
- Orkonerei Community Video (Ilaramatak Lorkonerei, Simanjiro): Wakiongozwa na Lukas Kariongi (ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Radio Orkonerei) aliyesimamia Sound, na Kassim Mustafa aliyekuwa mpiga picha na Editor.
- World Village Television (Maweni Farm, Lushoto): Walioshirikiana katika kutoa taswira hii adhimu.
Kwanini Wimbo Huu Hauna Mbadala Kwangu?
Tunapoufunga mwaka, wimbo huu unatukumbusha kuwa si kwa akili zetu, si kwa utajiri wetu, wala si kwa ujanja wetu tumefika hapa. Ni kwa neema tu.
Wadau wa Jamii Forums, tukumbushane... Nikienda kanisani mwisho wa mwaka hivi kwaya nyingi za watu wazima lazima ziupige huu