Kumbukizi ya Miaka 40 ya Kifo cha Sokoine

Kumbukizi ya Miaka 40 ya Kifo cha Sokoine

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine imenikumbusha historia ya rafiki wa Sokoine Mzee Ali Mohamed Mead.

Mzee Ali Mohamed Mead alikuwa mfanyabiashara mkubwa na akifahamika Masaini kote na alitajirika katika biashara.

Mali hii aliitumia bila choyo wala khiyana katika kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Mzee Mead alifanya mengi lakini kubwa ambalo linastahili kukumbukwa sana ni kutoa nyumba yake Monduli kuwa ofisi ya TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mali hii aliitumia bila choyo wala khiyana katika kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Miaka michache iliyopia mmoja wa watoto wa Mzee Mead baada ya kusoma makala nilizoandika kuhusu wapigania uhuru waliosahauliwa aliniletea picha ya baba yake akiwa kwenye foleni ya kupiga kura akiwa na Edward Sokoine.

Kampeni za uchaguzi Monduli zilikuwa zinaanzia nyumbani kwa Mzee Mead na baada ya hapo ndipo zinapelekwa kote kwa wananchi.

Huu ulikuwa uchaguzi wa mwaka wa 1980.

Picha ya kwanza inamuonyesha Sokoine amemtamguliza mbele Mzee Ali Mohamed Mead ili awe mtu wa kwanza kupiga kura kwa kutambua mchango wake katika chama.

Picha ya pili inamuonyesha Mzee Ali Mohamed Mead(aliyevaa hegal) akimpongeza Edward Lowassa baada ya kushinda ubunge uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995 na kuwa Mbunge wa Monduli.

1712871729095.png

1712871790055.png
 
Asante kwa historia
Tusubiri watuletee na historia ya babu yake mwamposa akimpaka maji ya upako Moringe wa Moringe...
 
Back
Top Bottom