Vile vile alikuwa mtangazaji mzuri sana wa soka michezo wa mpira wa miguu, nikimfananisha na magwiji wa RTD, kama vile Hamed Jongo na Dominic Chilambo.
Msome hapa moja ya kazi zake enzi hizo, akitangaza soka.
Kadenge na mpira, Kadenge na mpira, anachenga, moja, anachenga mbili, anakuja katikati, anaenda upande huu, anarudi upande mwingine, anakimbia, anatembea, anatambaa, anamvisha kanzu, anapepeta mpira, amemchenga mchezaji wa kwanza, amempita swipa, anamhepa fullback, mtizame, ndiye huyo, ndiye huyo, anaenda, anaenda, anaangilia huko, anaangalia kule, anatizama kushoto haoni mtu, anatazima kulia, zii mtu, atafanya nini, sasa mwangalie, anaajiitayarisha, anavuta, anapiga teke, anapiga shoot! anapiga shoot! anapiga shoot! mpira umepita moja kwa moja katikati ya miguu ya golkipa maarufu James Siang'a umeiingia ndani na kupasua wavu... wasikilizaji, wananchi, mashabiki, ni....gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!! gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!! gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!! gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!!
Tatu Bila!! Mayowe!! Kelele! Mashabiki wa Gor Mahia wamefurahi! Mashabiki wa Abaluhyia wamezirai!
Ah ah ah huyo ndio alikuwa Mzee Leonard "Mambo" Mbotela