Kumbukumbu kutoka Blantyre, Scotland kijiji cha David Livingstone 1991

Kumbukumbu kutoka Blantyre, Scotland kijiji cha David Livingstone 1991

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU KUTOKA KIJIJI CHA DAVID LIVINGSTONE BLANTYRE, GLASGOW SCOTLAND 1991

Hayo niliyoandika hapo chini nimemwandikia rafiki yangu Dr. Harith Ghassany mwandishi wa kitabu maarufu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' (2010):

Nilipokuwa Cardiff 1991/91 nilikuwa kila likizo nikienda kwa kaka yangu Glasgow, Scotland.

Hivi ndivyo nilivyoweza kufika kijiji cha Blantyre alikozaliwa David Livingstone.

Nilifanya kipindi BBC kutokea studio za BBC Glasgow kuhusu David Livingstone anuani ikiwa, ''Barua Kutoka Glasgow.''

BBC Bush House, London wakini - rekodi moja kwa moja kutoka Glasgow.

Pale Bush House marehemu Mlamali Adam alikuwa akifanya kipindi, ''Barua kutoka London," kikirushwa kila Jumamosi jioni.

Sasa nilipofika mimi wakanipa kipindi kimoja kutoka Glasgow.

Hiki kijiji chote cha Blantyre kimefanywa kumbukumbu na kimehifadhiwa kama kilivyokuwa wakati wa Livingstone.

Kila kitu chake utakiona hapo kuanzia shajara zake, vitabu alivyoandika, nguo zake nk. nk.

Katika kipindi kile nilieleza kuwa Mikindani nilifika Soko la Watumwa ambalo David Livingstone alishuhudia mnada wa watumwa akiwa amekaa pembeni yake na aliyoyaona hapo yalimsikitisha sana na akapeleka taarifa Uingereza kama ilivyokuwa kawaida.

Hili soko sijui kama bado lipo kwani nilipoliona mimi katika miaka ya 1980 mwishoni lilikuwa taabani.

Utakumbuka kuwa mwaka wa 2016 uliniletea taarifa kadhaa kuhusu hii kadhia ya Utumwa Zanzibar nyingine ukiandika wewe mwenyewe na nyingine wakiandika watu wengine.

Nimeingia Maktaba baada ya kusoma hii makala uliyoniletea na nimeikuta makala ya Zahir Al Kharusi ambayo nitakuwekea "link" hapo chini lakini hapa nataka usome kipande kidogo alichandika kuhusu David Livingstone:

''Kwa hivyo eneo hilo halikuwa na jengo la kanisa nyumba za mapadri wala hospitali majengo yote hayo yameasisiwa baada ya miaka ishirini kupita.

Maneno na historia inayotolewa kuwa palikuwa na soko ama nyumba iliokuwa ikifungiwa watumwa ni hadithi ya uongo na uzushi lengo lake ni kupandikiza chuki kubwa juu ya Uislamu na Waarabu wakati huyo David Livingstone huko kwao Uingereza na Marekani ndio walinunua watumwa zaidi ya milioni kumi kutokea nchi za Afrika.

Hapo Mkunazini ulikua uwanja mtupu uliopakana na sehemu ya mnada wa vitu vya kawaida yaani sokoni na ikawa ni urahisi mtu anayetaka kuuza mtumwa wake ampeleke eneo hilo lilopakana na sokoni amuuze.

Hakika nyumba iliokuwa chini ina eneo la chini la baraza na mfano wa vyumba vya chini lilikuwa linatumika kuwekea madawa yaliyohitajia ubaridi na usalama zaidi wa maradhi ya ndui (smallpox diseases) yaliowahi kuwepo miaka ya 1910-1920 hapa Unguja.''

Picha ya kwanza sanamu ya David Livingstone, Glasgow picha ya pili nikiwa Blantyre na ya tatu niko BBC Glasgow nikifanya kipindi cha David Livingstone mwaka wa 1991.


Screenshot_20220331-170530_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom