Kumbukumbu ya jumba ya Mwalimu Nyerere wanatafiti historia ya awali ya Baba wa Taifa

Kumbukumbu ya jumba ya Mwalimu Nyerere wanatafiti historia ya awali ya Baba wa Taifa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WATAFITI KUTOKA KUMBUKUMBU YA NYUMBA YA MWALIMU NYERERE MAGOMENI WALIPONITEMBELEA

1569603088879.png

Jana Maghrib mimetembelewa na maofisa wawili kutoka Kumbukumbu ya Nyumba ya Mwalimu Julius Nyerere, Bi. Gilago Victoria na Bi. Nathalia Joseph wakitaka niwape historia ya siku za mwanzo za Baba wa Taifa.

Tumerekodi video ya karibu saa nzima.

Nimewaeleza historia ya Mwalimu kuanzia siku ya kwanza alipofika nyumbani kwa Abdulwahid Sykes akiwa kaongozana na Joseph Kasella Bantu mmoja kati ya watu 17 walioasisi chama cha TANU mwaka wa 1954.

Watafiti hawa walishangaa sana nilipowaeleza kuwa mzalendo aliyekuwa mpangaji wa mipango ya kumuondoa mkoloni Tanganyika na akatafuta viongozi wa kutekeleza azma hii alikuwa Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962).

Nikawafahamisha kuwa Mwapachu kwa vijana wote aliokuja kuwaingiza katika harakati hizi kuanzia, Abdul Sykes, Julius Nyerere, Paul Bomani na wengine wengi kama akina Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi yeye alikuwa ni ''Kaka Mkubwa,'' kwao kwani aliwapita kwa umri kwa zaidi ya miaka 10.

Tukazungumza jinsi Mwalimu Nyerere alivyoingizwa katika uongozi wa TANU mwaka wa 1953 katika mkutano wa mwaka wa TAA uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo baada ya mazungumzo ya kumjadili kufanyika nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu, Nansio Ukerewe kati ya Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Walitaka kujua maisha ya Mwalimu alipoacha kazi na kuja kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes kabla ya kuhamia Magomeni Majumba Sita mwaka wa 1955.

Hawa dada zangu walitaka sana kujua historia ya Mshume Kiyate na Mwalimu Nyerere ambayo niliwaeleza.

Lakini kisa ambacho naona kiliwagusa sana ni kile kisa ilidhaniwa kuwa Mwalimu kalishwa sumu nyumbani kwa Abdul Sykes kukatisha maisha yake.

Hii ilikuwa katika moja ya zile ''retreats'' mashuhuri ya ile Kamati ya Ndani ya Kamati ya TANU (Inner Circle) ya Nyerere Abdul, Ali, Dossa na Mzee Rupia na viongozi wengine wachache walikuwa wakifanya nyumbani kwa Abdul Mtaa wa Aggrey na Sikukuu kila walipokuwa na jambo muhimu la kujadili.

Walitaka kujua kama nyumba hii ingalipo nikawafahamisha kuwa imevunjwa miaka mingi na sasa hapo kuna gorofa ndefu kama ilivyo ada ya Kariakoo siku hizi.

Watafiti hawa waliuliza kama ipo picha ya nyumba hiyo.

Niliwafahamisha kuwa picha ipo lakini si ya nyumba ile ya Nyerere na Abdul bali ipo ambayo nyumba imefanyiwa marekebisho.

Walinifahamisha kuwa hapo na mahali muhimu sana katika historia ya Baba wa Taifa na uhuru wa Tanganyika na wangependa kuweka alama ya kumbukumbu.

Naamini hawa dada zangu waliifurahia sana historia hii.

Picha ya kwanza na ya pili nawaonyesha picha ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 1962 Nyerere akiwa na Mshume Kiyate, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi, picha ya tatu ni Hamza Kibwana Mwapachu.

 
Kaka Moh'd hili la suala la sumu ilikuwaje na nani alihusika.
 
Kaka Moh'd hili la suala la sumu ilikuwaje na nani alihusika.
Nnangale,
Ukweli ni kuwa hapakuwa na sumu yoyote katika kile chakula ni bahati mbaya tu tumbo lilimpinduka Mwalimu Nyerere na rafiki zake wakataharuki kwani hiyo ni hofu wakiishi nayo siku zote kuwa kuna maadui wanamuwinda Nyerere.
 
Back
Top Bottom