Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUMBUKUMBU YA KUMBUKUMBU YA KARUME DAY MAHOJIANO: "THE MASTERMIND" MAHOJIANO NA IRENE KILENGA AZAM TV MORNING TRUMPET 2015
Tuanze na picha ya Mzee Karume akiwa na vijana wa mji wa Dar es Salaam katika miaka ya 1940 kudhihirisha kuwa Abeid Amani Karume hakuwa mgeni wa mji na akifahamiana na wana mji kindakindaki.
Picha hiyo ya kwanza ilipigwa Dar es Salaam mwaka 1948.
Kushoto waliokaa Hassan Machakaomo, Selemani Mwinyimadi Chambuso, Mohamed ''Mabosti'' Sultan.
Huyu Hassan Machakaomo baba yake Mzee Machakaomo alikuwa Mzulu aliingia Tanganyika na Herman Von Wissman mwishoni mwa 1800 kama askari mamluki pamoja na akina Affande Plantan na Sykes na wakaishi jirani Mtaa wa Kipata.
Mohamed Sultan alipewa jina la ''Mabosti,'' kwa ajili ya unadhifu wake katika mavazi na mbwebwe zake za kijana mtanashati.
Mohamed Sultan alipata kuwa President wa Young Africans.
Waliokaa kwenye viti kushoto wa kwanza jina halikupatikana, Rajab Swedi, Khamis Shari, Abeid Amani Karume, Kondo Salum Kipwata, Mtaruke Mangara, aliofuatia jina halikupatikana.
Kondo Kipwata inaaminika ndiye Mwafrika wa kwanza Dar es Salaam kununua radio wakati utangazaji wa radio ulipoanza mwaka wa 1952.
Watu walikuwa wakikusanyika barazani kwake Ilala kumsikiliza Yahya Hussein wakati huo mtoto mdogo akisoma Qur'an kupitia Sauti ya Unguja.
Kondo Kipwata alikuja kuwa President wa Young Africans katika miaka ya 1960 tena kwa kulazimishwa na wanachama na wapenzi wa Yanga baada ya kuwa kila mechi wanafungwa na mahasimu wao Sunderland.
Kondo Kipwata alikuwa haendi kuangalia mpira wa Yanga na Sunderland akisikiliza nyumbani kwake kwenye radio.
Mjukuu wa Affande Plantan na mtoto wa Mwalimu Thomas Plantan, Bi. Maunda Plantan alikuwa mwanamke wa kwanza kutangaza Sauti ya Dar es Salaam tena alikuwa English Service.
Waliosimama Abdallah Mzee, Chonjo Mwinchande Digendo, Juma Ismail, Shaaban Bajuni, anaefuatia jina halikupatikana, Khamis Mjinga, Selemani Mohamed, Mtoro Rehani, Mangara Tabu Mangara na Ali Majaliwa.
Mangara Tabu alikuwa President wa Yanga katika miaka ya 1960 mwishoni hadi 1970 mwanzoni na katika uongozi wake Yanga ilifanya makubwa pamoja na kujenga club hiyo iliyopo Jangwani kwa msaada wa Karume.
Mwangalie Mangara Tabu na Karume utaelewa urafiki wao umetokea wapi.
Picha ya pili hapo ni asubuhi (7 Aprili, 2015) nikifanya Kipindi Maalum cha Rais Abeid Amani Karume (1905 - 1972) "The Mastermind," na Irene Kilenga wa AZAM TV.
Kipindi kilikuwa cha takriban saa moja na nilieleza maisha ya Karume kuanzia mwaka 1955 alipohudhurua mkutano wa kwanza wa TANU uliofanyika Ukumbi wa Hindu Mandal Dar es Salaam ambako alikutana na Mwalimu Nyerere na Karume akamualika Nyerere Zanzibar.
Nilieleza pia hiyo haikuwa ndiyo mwanzo wa kukutana.
Walikutana kabla Zanzibar baada ya TANU kuundwa mwka wa 1954 wakati Abdul Sykes na Dossa Azizi walipompeleka Nyerere Zanzibar kumtambulisha kwa Karume akiwa na Mtoro Rehani.
Mtangazaji wa AZAM TV Irene Kilenga alivutiwa sana na jina nililompa Mzee Karume - "The Mastermind," na alitaka kujua zaidi ni kipi kilinifanya mimi kumpa jina hilo.
Nilimpa kisa chake toka mwanzo 1954 hadi kumalizikia kuuliwa kwake mwaka wa 1972.
Baada ya mahojiano ndani ya studio AZAM TV waliomba tufanye kipindi cha nyongeza kuhusu Mzee Karume nje ya studio.
Staili ya vipindi hivi nilikuwa naeleza historia ya ndani ya hali ya Zanzibar kutokana na hali halisi kama nilivyokuwa nikisikia rafiki wa baba yangu wakizungumza na baba nyumbani nami nikiwepo lau ni mtoto nilikuwa nahisi haya ni mambo mazito.
Nakumbuka kifo cha Abdulaziz Twala na Jaha Ubwa hawa walikuwa marafiki wakubwa wa baba yangu.
Namkumbuka na Bwana Yunus yeye alikuwa Jeshi la Polisi na akimtembelea baba kutoka Zanzibar mara nyingi.
Nikisikiliza mazungumzo yao na sikujua wakati ule kuwa haya mazungumzo ni darsa katika kuwajua Wazanzibari na historia yao.