Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

2


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko mimi kwa nia njema kabisa nakusihi nisikilize. Kuna makosa makubwa unayaandika katika historia ya TAA. Dr. Kyaruzi alihamishiwa Kingolwira lakini ilipoonekana kuwa kila weekend yupo Dar na Abdul Sykes akapelekwa Nzega. Huu ni mfano mmoja. Hakuna Sheikh katika mji wa Dar es Salaam ambae mimi sina historia yake. Huyo Sheikh Issa unaemtaja katika TAA hakuwapo. Mimi nakushauri tu kwa nia njema maana ukiendelea hivyo unakiua kitabu chako ikiwa kitakujafanyiwa "review" na mjuzi wa historia ya Tanganyika. Makosa yako mengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko nimeona umebadilisha uhamisho wa Kyaruzi. Kwanza ulisema Sengerema sasa umegeuza umeandika Kingolwira. Unasema rais wa kwanza TAA alikuwa Kyaruzi. Nishakueleza TAA hakikuwa chama kipya ni jina tu lilibadilika 1948 na rais alikuwa Thomas Plantan. Mwanae Bi. Mwalimu Maunda yu hai na anasoma, anaandika na kusema Kiingereza vizuri tu. Anaijua vyema historia ya baba yake. Mpe mhariri apitie kazi yako itakaa vyema. Kitu muhimu katika kitabu ni, "facts," ambazo wewe hunazo.


Mwalimu Maunda Thomas Plantan na Mwandishi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko kisa cha kuibadili TAA kuja TANU kimeelezwa vizuri na Judith Listowel katika kitabu chake, "The Making of Tanganyika," Chato and Windus 1965. Haiko kama unavyohadithia. Zipo barua kadhaa kati ya Listowel na Ally Sykes mimi nimezisoma na kufanya rejea. Huyu mama alijulishwa kwa Ally Sykes na Peter Colmore na ndiye aliyemsaidia kumpitisha kote kufanya utafiti. Angalia kitabu cha Abdul Sykes habari zote hizi zimeelezwa. Kwa ufupi inner circle ya TAA Abdul, Ally, Nyerere, Dossa, Rupia ndiyo waliamua kuja na TANU na kichekesho Listowel anaeleza kuwa hata viti vya kukalia havikutosha mle ndani ya ofisi ya TAA, New Street. Hakuna mzee wa Dar es Salaam alikuwapo hawa walikuwa wameshataarifiwa huko nyuma baada ya TAA kudhoofika Nyerere aliopochukua uongozi. Dossa kaeleza haya. Angalia video niliyoweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa mara nyingine nakukumbusha ndugu yangu Yericko Nyerere huu mjadala ni wa muhimu sana, basi ujitahidi kuandika vitu vyenye fact kwa faida ya wasio elewa, unapoandika makosa basi wasomaji wasio na uelewa wa hayo mambo wanayachukua hayo makosa
Hivi unawezaje kuwahusisha Jesuits na Maryknoll sisters? Iweje Maryknoll sisters wawe shirika tanzu la Jesuits wakati hao Jesuits hawana affiliation na shirika lolote la masista?
 
Kituko,
Yericko
ngewasoma Jesuits angewajua.

Huwa nampuuza kisha ubinadamu hunijia na kusema hapana
nina dhima ya kumsahihisha ili kazi yake ikae vyema nikikaa kimya ni
sawa na kumfanyia khiyana.

Anasema baada ya kifo cha Cecil Matola, Kleist alikaimu nafasi yake
ya urais.

Haikuwa hivyo alipofariki Matola, Mzee bin Sudi akachaguliwa kuwa
rais.

Hiki kipindi cha Mzee bin Sudi ni muhimu maana ukimsoma Kleist
mswada wake utaona ni kipindi kilikuwa na mapambano sana kati
viongozi wa AA kiasi Kleist alijiuzulu uongozi baada ya kugombana na
Erika Fiah.


Erika Fiah

Yericko
anatumia lugha za ovyo ''wahamiaji haramu.''

Angesoma historia ya ukoloni angeona jinsi Waafrika walivyokuwa
wanaingia nchi na nchi kirahisi bila shida.

Dome Budohi Mluya kutoka Kenya alikuwa kiongozi wa TAA na akawa
mwanachama wa TANU kadi no. 6.


Mwandishi na Dome Budohi, Ruiru Nairobi 1972

Dennis Phombeah mwanachama wa TAA na TANU na yeye Mnyasa.
Mifano iko mingi sana.
 
Huenda nikaonekana silifahamu jambo la Udini katika TANU,ila haipingiki kuwa TANU imekuja baadaye ila Mtizamo wa Udini ulishajengeka ukajengeka,ni Mwalimu JK ndiye alipambana nayo.
Huyo Takadir uliyemtaja hakuwa pekee yake yeye alikuwa kama Msemaji anawawakilisha watu majabali.

Hata wewe Mzee wangu ni Shahidi kuwa hata maelezo yako ya historia huwa Una-base sana kwenye Udini kiasi unakuwa makini kuelezea Waislam walioshiriki Uhuru kuliko Wakristo na ndiyo maana Vyombo unavyotumia ni vya Kiislamu mfano Radio/Tv Imaan na Kitabu chauzwa Misikitini zaidi kuliko pengine Msikiti wa Manyema,Msikiti Ngazija,Msikiti Mtaa wa Lindi,Gerezani.


Haipingiki pia kuwa Marehemu Abdulwahid Sykes alikuwa ni Mdini pia na ilichangia kusigana na Mwalimu.Hata unapotoa maandishi yako huliweki hili, kuna Member kaiongelea AMNUT ambayo Sykes alikuwa na mkono nayo,cha ajabu Mzee wetu huiongelei hoja hii japo iko wazi.Kuyajua haya rejea wapingaji wanoipinga Bakwata ndiyo utaielewa historia ya "Wadini wa Uhuru" .

Mwanahistoria mzuri huwa haegemei Upande.Kiasi leo hii hata kuandika ukweli kuwa Kanisa Anglikana Zanzibar lilichangia kununua Watumwa ambao wakawa wanawaacha huru na kuwa chanzo cha kuua biashara hiyo,na chanzo cha kuitwa Mission Quarters kwa historia ya Watumwa wa Zanzibar, hapo jirani kwa Marehemu John Rupia. Haisemwi.

Kuna mengi sana Wanahistoria wa Kiislamu huangalia mambo Kiudini.

Kuna Wakristo wengi mno walifanya makubwa nchi hii,hawaongelewi na wala haiwi shida nimejaribu kuangalia Video zako nyingi Mzee wangu upo hivyo,asipoandikwa au kupewa kipaumbele Muislam/Uislam huwa unaongea katika hali ya Masononeko Makuu.

Kikubwa huwa napenda kujifunza hasa Ukweli.Na hupenda kukosolewa na Kukosoa pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ligema274,
Nisingependa kuingia katika mjadala huu na kubwa jinsi kutokana
na unayoandika inaelekea huna ulijualo katika somo hili.
 
Unakosoa wewe, unakubaliana wewe, unazungumza wewe basi kila kitu ni wewe...
 
Kabla hujaingia kwenye hiyo unayoita kunikumbusha, nakusihi jipe muda kutafuta taarifu na kuzisoma na kuzielewa...

Kaisome Jeisuti ni nini na ipo kwaajili ya nini? Kasome mashirika tanzu ya RC... Kija njoo ukae ufunzwe hapa mkuu... Juu ya haya ninayo ya kuwafunza wengi kuliko mimi kujifunza...
 
Unaathiriwa na tatizo moja hatari sana, hutaki kupokea jambo lolote mpya kwako.... Hasa liwe mpya linalovuruga lile uliloliamini.
 
Nina kusihi mzee wangu, uwe tayari moyo na akilo yako kupokea mambo mapya katika historia ya Tanganyika,

Nakumbuka kule nyuma ulisema yote niliyoandika nimekopi kwako na kwamba hakuna mpya, je haya ya Jeisuti kuratibu mtu wa kushika madaraka ya nchi na kumlea Julius kuanzia utoto wake mpaka kumpeleka TAA na hatimaye kumkabidhi nchi hili ulilijua?

Tambua hilo ndio mpya katika kitabu hiki...
 
Yericko,
Hakuna tatizo ulikuwa ni ushauri.
Aliyezungumza kuhusu Jesuits si mie ni Kituko.

Mimi nimesema uwasome Jesuits ili uwafahamu.

Hilo lingine ulilosema wala si jipya limekuwa katika midomo
ya watu kwa miaka mingi sasa ila hapana ushahidi na bila ya
ushahidi mtu hulitii jambo katika maandishi.

Ilitaka na wewe uweke, ''source,'' ya kuaminika ndipo utaaminika
ikiwa umekusudia hii kazi yako ni ya kisomi.
 
Yericko,
Hakuna tatizo ulikuwa ni ushauri.
 
Unakosoa wewe, unakubaliana wewe, unazungumza wewe basi kila kitu ni wewe...
Yericko,
Hayo ni makosa nimeyaona ikiwa unaona uko sawa hakuna shida.

Mimi kadri utakavyosema katika somo hili nimefanya utafiti na kuja
na kitabu ambacho kipo na kinasomwa.

Hili halikwepeki.

Hata mathalan ikiwa atatafutwa mtu wa kufanya ''review,'' ya kitabu
chako usishagae nikawa mimi.
 
Sources zote zipo kwenye kitabu yaani nyaraka zote... Jipe muda mzee wangu ukisome kitabu hiki
 
Hahahaaa asante sana... Review si kama pombe za ngomani maalim.

Nitafurahi ukiwa wewe kwakuwa ninakuwa tayari nina matokeo ya review yako hata kabla ya kukamilisha review yenyewe....

Umepata chain ya Uhuru wa Tanganyika, Julius Nyerere, Kanisa katoliki, Kanisa Anglikana, Malkia Elizaberth, wazee wa Dar na UNO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…