Kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha Abdul Sykes

Kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha Abdul Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA KIFO CHA ABDUL SYKES

Ile kamati ndani ya kamati katika TAA ya Abdul Sykes, Ally Sykes John Rupia na Dossa Aziz walikuwa wameshakubaliana kuwa Nyerere lazima achukue ile nafasi ya rais na mwaka unaokuja 1954 wanaunda TANU. (Kamati kubwa ni ile TAA Political Subcommittee ya Sheikh Hassan bin Ameir iliyoundwa 1950).

Hii ni baada ya Abdul kutoka Nansio kwa Hamza Mwapachu na Hamza kumpa kauli yake kuwa Nyerere apewe uongozi na TANU iundwe 1954 udaiwe uhuru. Unajua Hamza kwa Abdul na Nyerere alikuwa ni mkubwa kwa kuzaliwa. Hamza kazaliwa 1913 na Nyerere 1922 na Abdul 1924. Angalia tofauti ya umri kati ya watu hawa. Kisha Hamza mambo haya kayajua mwanzo. Alikuwa kawazidi kwa kila hali. Inasikitisha sana kuwa historia imewaruka watu muhimu sana katika historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru. Lakini jambo hili la kumwingiza Nyerere halikuwa la kutangazwa kila mwanachama akalijua kuwa sasa akina Abdul wanaunda chama cha siasa. Ilikuwa siri. Juu ya haya Denis Phombeah yeye hakuwa katika ile duru ya ndani kwa hiyo yeye akawa anamfanyia Nyerere kampeni amuangushe Abdul na Abdul akawa anamtazama tu hafanyi lolote kwani hicho ndicho kilichotakiwa. Juu ya haya Nyerere alishinda kwa kura chache sana katika uchaguzi ule. Tena uchaguzi huu ulikuwa wakionyesha mikono. Jambo la kusikitisha historia hii ni kama vile inatisha hata Nyerere mwenyewe hajapata kusema vipi alijuana na Abdul nini walikuwa wakipanga katika kuunda TANU nk. nk.

Kuna kitu kimoja muhimu sana. Unajua Abdul yeye alitaka Chief Kidaha Makwaia wa Siha aje TAA wamchague rais na kisha waunde TANU na mazungumzo haya yao hayakuwa na mafanikio ikawa kama vile Abdul amepwelewa ndipo Hamza akaja na jina la Nyerere. Lakini kama mwaka ule 1953 hii Inner Circle ya TAA ya akina Abdul wangefanya khiyana ya kumkataa Nyerere kwa sababu yoyote ile wangekuwa wamefanya kosa kubwa sana. Uhuru usingepatikana 1961. Abdul alikuwa amekifikisha chama pale alipolifikisha na hakuweza kukipeleka mbele zaidi ya hapo yeye akiwa kiongozi wa juu. Huu ndiyo wakati Earle Seaton akimsukuma sana Abdul aende Princeton University, New Jersey kusoma na admission letter alikuwa tayari anayo mkononi. Ukisoma Nyaraka za Sykes za 1953 utaona mambo yalikuwa mengi sana na hiki ndicho kipindi serikali ikitoa circular za kutisha. Huu ndiyo mwaka Kamati ya Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes ilikuwa inazunguka Tanganyika kueleza dhulma za Ardhi ya Wameru. Abdul alikuwa karibu apoteze kazi yake ya Market Master Kariakoo Market.

Abdul alikuwa amekifikisha chama pale alipolifikisha na hakuweza kukipeleka mbele zaidi ya hapo yeye akiwa kiongozi wa juu. Huu ndiyo wakati Earle Seaton akimsukuma sana Abdul aende Princeton University, New Jersey kusoma na admission letter alikuwa tayari anayo mkononi. Nadhani unaona TAA ilikuwa kwenye stalemate.Hamza Mwapachu alikuwa mwamba unajua hapo alikuwa keshasoma medicine na kaacha kutibia akaenda University of Wales, Cardiff kusoma Social Science. Huyu ndiyo alikuwa hirizi yao hawawezi kumpinga walikuwa wanamuamini sana. Hamza wakati ule yeye anaandika makala katika gazeti la Sentinel za Fabian Society. Hawa Fabian ndiyo walikuwa siasa kali katika Labour Party ya Uingereza. Ninazo nakala za barua za miaka ya 1940 mwishoni Mwapachu akiandikiana na viongozi wa Fabian Society. Inasikitisha kuwa historia hii tulitaka kuicha ipotee bure.
 
Hapa Kazi tu.
Mababu zetu Walienda Ulaya huku Wanalia , Ila sisi tukipata Viza tunashangilia.
R.I.P Langa.
 
GRIMSHAW.jpg




Sunday News 20 October, 1968

Abdulwahid alipofariki Wizara ya Habari ilitoa taarifa ikieleza kuwa Rais Nyerere amehudhuria maziko ya Abdulwahid Sykes. Kingine kinachostaajabisha ni kuwa taarifa ile ilitoa maelezo machache ya uajiriwa wake katika serikali na kuacha maelezo muhimu ya Abdulwahid katika siasa. Ilikuwa Mwingereza, Brendon Grimshaw, mhariri wa Tanganyika Standard, ndiye aliyempa Abdulwahid heshima na hadhi anayostahili baada ya kifo chake kwa kuchapisha taazia ambayo ilimweleza Abdulwahid kama: ‘’mmoja wa wapangaji wa vuguvugu la kudai uhuru na mmoja wa watu waliomsaidi Nyerere kuingia katika siasa.’’

Taazia ile ilitoa sifa kemkem kwa ukoo wa Sykes katika kuleta maendeleo ya siasa Tanganyika kwa kusema kuwa, ‘’msukumo mkubwa wa Waafrika wa Tanganyika kupata chama cha siasa chenye nguvu ulitokana na juhudi za ukoo wa Sykes.’’ Inasemekana taazia hii iliyompa marehemu Abdulwahid heshima na sifa za uzalendo wa hali ya juu iliwaudhi baadhi ya viongozi katika TANU. Viongozi hao wakawa wakisikika wakisema kuwa Ally na Abbas Sykes walikuwa wanajaribu kumtukuza kaka yao.
 
1539084525098.png


Halafu watu wanalalamika askari kuwa na kadi za chama. Hayati Sykes (R.I.P) alishatuonyesha mfano.
------
Nikirudi kwenye mada
Inasemekana taazia hii iliyompa marehemu Abdulwahid heshima na sifa za uzalendo wa hali ya juu iliwaudhi baadhi ya viongozi katika TANU. Viongozi hao wakawa wakisikika wakisema kuwa Ally na Abbas Sykes walikuwa wanajaribu kumtukuza kaka yao.
Mkuu, kwenye mambo kama haya; unapotoa tuhuma za wakati huo (tuhuma siyo ukweli) hata kama ungekuwa ukweli basi jitahidi kutoa na kauli za nyongeza za suluhu ya kupatanisha kati ya ndungu marafiki na taifa kwa ujumla hasa ya wale waliokuwa wanatuhumu na kutuhumiwa. Kurejea historia kama hii bila kurejea 'spirit' ya maridhiano na mapatano sisi wenye kufikiri kwa 'wastani' tutasema , Hapa mkuu unaibua uchochezi. Nina imani ushauri wangu huu utakukuta ukiwa bhuheri wa afya na utautazama kwa 'jicho' la tatu. Natanguliza shukrani kwa kusoma maoni yangu na kuyaelewa.
 
View attachment 891816

Halafu watu wanalalamika askari kuwa na kadi za chama. Hayati Sykes (R.I.P) alishatuonyesha mfano.
------
Nikirudi kwenye mada

Mkuu, kwenye mambo kama haya; unapotoa tuhuma za wakati huo (tuhuma siyo ukweli) hata kama ungekuwa ukweli basi jitahidi kutoa na kauli za nyongeza za suluhu ya kupatanisha kati ya ndungu marafiki na taifa kwa ujumla hasa ya wale waliokuwa wanatuhumu na kutuhumiwa. Kurejea historia kama hii bila kurejea 'spirit' ya maridhiano na mapatano sisi wenye kufikiri kwa 'wastani' tutasema , Hapa mkuu unaibua uchochezi. Nina imani ushauri wangu huu utakukuta ukiwa bhuheri wa afya na utautazama kwa 'jicho' la tatu. Natanguliza shukrani kwa kusoma maoni yangu na kuyaelewa.
Tujitegemee,
Mimi sijaelewa kuhusu ''tuhuma,'' unazozingumza.
Nimeeleza yale yaliyotokea wakati ule na ni kweli ndivyo ilivyokuwa.

Lakini kama unahisi ningeweza kuboresha niliyoandika hebu nipe
mfano vipi ningeliandika.

Kukosea ni silka ya binadamu na kufunzana ndiyo njia nzuri ya
kutengeneza palipoharibika.

Nani pia natanguliza shukurani kwa kusoma maoni yangu na kuyaelewa.
 
Back
Top Bottom