junky
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 413
- 978
1.Ntwadumela ni neno la kisavuti lenye maana ya "He who greets with fire".Katika msitu wa savuti uliojaa miti,wanyama na mto ukikaribia kufika utakutana na kibao kilichoandikwa " He who greets with fire" maana ya kwamba salamu utakayopewa itaambatana na moto...Ni simba dume mwenye umbile kubwa na misuli iliyotanuka na kimuonekano anavutia hakuna simba jike asiyependa kuwa na mwanaume kama Ntwadumela almaarufu "He who greets with fire" ambaye ana sifa kedekede ya utanashati na ngozi,nywele,taswira inayovutia na ukimuona bila kupepesa macho utagundua huyu kweli ni mfalme wa nyika.
2.Ntwadumela kama linavyojisanifu jina lake "He who greets with fire" ni kwanini simba huyu dume alipewa jina hili?
Ntwadumela anasifika kwa ukali uliotukuka kwa lugha ya mtaani hana mswalia Mtume,ukijifanya wewe ndio mtoto wa mjini ,jeuri basi pasi na shaka utapewa salamu na salamu yenyewe sio ile ya shikamo bali ni [emoji91][emoji91].
Wanyama walikuwa wanamuogopa Ntwadumela kwenye msitu wa Savuti na Ntwadumela alikuwa anamiliki eneo lake "territory" kama simba dume wanavyofanya na ukiingia kwenye eneo la Ntwadumela inabidi uingie kwa unyenyekevu na kwa sauti ya chini ila ukijifanya kupiga kelele basi utaamsha ghadhabu ya Ntwadumela na hakika hautokuwa salama,moja ya sifa ya Ntwadumela akikukasirikia hutoa mngurumo na base na kuanza kitroti kukufuata huku macho yake yakitoa taswira ya hasira aliyonayo na akikukimbiza omba sala yako ya mwisho sababu huwa hakati tamaa na mpaka ahakikishe amakumaliza.
3.Fisi walikuwa wanamuogopa Ntwadumela na fisi kama inavyozoeleka tabia yao hutembea kwa kikundi na hupenda kuwa bughudhi simba kwa makelele na matani mengine lakini kwa Ntwadumela walikuwa wanakaa mita 200 na wakimuona anajitokeza basi hukimbia kuhofia maisha yao na Ntwadumela alikuwa na allergy na fisi kila akiwaona fisi nafsi yake huchefuka na fisi kwa kuligundua hilo kwenye msitu wa savuti wakawa kila wakimuona hukimbia kwa kuhofia kupewa salamu ya [emoji91][emoji91]
4.Ntwadumela alikuwa na kaka yake wa tumbo moja aitwaye mandevu kama wanafalsafa wasemavyo tabia za ndugu hufanana huyu mandevu nae alikuwa mtata sana na alikuwa anapenda kutembea na kaka yake Ntwadumela,kwa muonekano mandevu alikuwa na mwili mkubwa kuliko Ntwadumela lakini Ntwadumela alikuwa na ujasiri mkubwa usio na kifani..baada ya Ntwadumela na mandevu kutawala ngome ile kwa muda mrefu wakaamua kuondoka na kumruhusu simba mmoja aliyekuwa mzee kukaa kwenye himaya ile na majike ,baada ya Ntwadumela na mandevu kuondoka na kutokomea zao wale simba jike waliobaki na dume mzee walipata shida sana kwenye uwindaji sababu yule mzee hakuwa na msaada kwenye kusaidia kuwinda wanyama wakubwa na pia amani na utulivu kwenye kikundi ikapotea na simba dume waliokuwa vijana wakagawanyika na kuondoka na kupotea mbali yule mzee alishindwa kusimama kama kiongozi sababu ya uzee wake na hatimaye wale simba jike kuna nyakati walikuwa wanakaa na njaa na wakiwinda wanawinda kwa desperate na wakati mwingine huumia sana hakika kuondoka kwa Ntwadumela ilikuwa pigo sana kwao.
5.Ntwadumela na mandevu walielekea kaskazini kwa mbali kidogo eneo lingine masikini ya mungu kumbe hawakujua kuwa walikuwa wanaelekea kufa ,wakati wapo safarini wakielekea pori lingine wakapita sehemu ambayo hutumika kifanyia uwindaji.Wazungu walimegewa eneo na serikali wawe wanawinda na masikini ya Mungu wawindaji wale wakammiminia risasi Ntwadumela wakijitetea kwa madai ya kwamba Ntwadumela alipowaona wale wawindaji na kama inavyojulikana neno Ntwadumela lina maana ya "He who greets with fire" wale wazungu walipewa salamu [emoji91][emoji91]
Wawindaji wale walikuwa kwenye gari ndipo Ntwadumela alikimbia na kumrukia mmoja wapo na ndipo hapo akamiminiwa marisasi kwa mujibu ya wawindaji wale na mchezo ukaishia hapo wahindi wanasema marighaya ,wahispaniola wanasema finito..Ntwadumela maisha yake yakaishia hapo simba aliyekuwa na sifa kedekede na aliyepata umaarufu wa "He who greets with fire"aliyekuwa na ubavu wa kupambana na tembo na kumuangusha na kusaidia kwenye kitoeo ,aliyekuwa anapambana na nyati na wanyama wengine wakubwa hakika alikuwa fighter na shujaa.
Na sio Ntwadumela aliyeuliwa pekee pia kaka yake mandevu aliuliwa na trophy hunters wale ,
Baada ya kuuliwa simba hawa ngozi zilipelekwa USA na watu/dunia ilisema sana na kuhuzunika sababu kifo chao hakikuwa cha uungwana kabisa.
Vipi kama wasingehama eneo lao na kuwakacha familia yao ya majike na watoto huenda wasingepoteza maisha na kukutana na risasi .