Kipindi hicho hapo juu nilifanya na TBC1 mwaka jana Nyerere Day 2021.
Shida kubwa iliyokuwa inanikabili katika maswali niliyoulizwa ni kuwa yalikuwa maswali yanayoitwa ''leading questions,'' yaani swali ambalo tayari lishakuelekeza ulijibu vipi.
Mimi nikawa nayakwepa haya maswali kwa kulitengeneza swali ili jibu langu liwe na maana zaidi.
Picha ya Mwalimu Nyerere kutoka Maktaba ya Picha ya marehemu Iddi Tosiri kadi yake ya TANU ni No. 25 ni mmoja wa waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU mwezi August 1954. Ndugu ya Iddi Faiz Mafungo (kadi No. 24) na Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo. Picha nimeipata kwa Maulid ''Chubby' Tosiri mtoto wa Iddi Tosiri.
Shariff Abdallah Omar Attas (mume wa Bi. Chiku bint Said Kisusa) katika umri ambao alifahamiana na Julius Nyerere Soko la Kariakoo. Shariff Attas alikuwa mkusanyaji wa ushuru wa nafaka hapo sokoni.
Kulia: Julius Nyerere, John Rupia na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na nyuma yao ni Bantu Group.
Rajab Matimbwa muasisi wa kwaya ya kwanza ya TANU New Street 1954.
Mzee Mohamed Said hongera sana kwa tuzo ya Stories of change 2021. Nimechelewa kukupa salamu hizi kwa maana sikuwa hapa JF kwa muda wa miezi 12 iliyopita.
Mzee Mohamed Said hongera sana kwa tuzo ya Stories of change 2021. Nimechelewa kukupa salama hizi kwa maana sikuwa hapa JF kwa muda wa miezi 12 iliyopita.