Kumbukumbu ya Ramadhani 6

Kumbukumbu ya Ramadhani 6

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUKUMBU YA RAMADHANI 6

Nimeona nieleza na mengine katika haya pamoja na kumbukumbu za Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sala ya Eid Kubwa Maputo, 1990
Kuhitimisha nakurudisheni Maputo mwaka wa 1990.

Nilisali Eid Kubwa Maputo.
Msumbiji Eid siyo sikukuu inayotambuliwa na serikali.

Waislam wako wengi tu lakini hiyo ndiyo hali.
Msikiti uko mjini kabisa na unajaa hadi nje.

Katika hali kama hii vuta hisia mathalan sala ya Eid Msikiti wa Ngazija ambao uko katikati ya mji na watu wanasali hadi nje wametandika mabusati lakini kwa kuwa ni siku ya kazi magari na watu wanapita pembeni watu wakisali wakiendelea na shughuli zao.

Hali kama hii ina raha yake kuishuhudia.
Ramadhani Berlin, Germany 2011

Mwaka wa 2011 nilikuwa Ujerumani kwa mwezi mzima na Ramadhani ikanikuta Berlin.

Berlin Waislam walio wengi ni Waturuki.

Jirani na nyumbani kwangu kuna mgahawa na kuna duka la vyakula na biashara zote hizi ni za Waturuki.

Katika mgahawa huu ndipo nilipokuwa nachukua chakula changu ''takeaway,'' ninapotoka ofisini kwangu nakwenda kula nyumbani.

Waturuki wanapika si mchezo.

Kama kesho Ramadhani nikauliza ratiba ya tarwehe kwenye msikiti wa jirani na mipango ya futari hapo mgahawani.

Katika nchi nilizojaaliwa kufika hakuna nchi ngumu kama Ujerumani.
Wajerumani muda wote sura zao kama jiwe.

Hawana tabasamu wala hawataki kusema Kiingereza wala vibao hawaweki tafsiri.

Ni juu yako wewe mgeni kujifunza lugha yao.

Mawasiliano yangu na Waislam wenzangu Waturuki yalikuwa ya shida sana lakini walipojua mimi ni ndugu yao walikuwa wakiniadhimisha sana ninapofika pale mgahawani au kwenye lile duka la vyakula.

Nimekwenda mgahawani kununua futari.
Mashaallah menu imeenea kazi kwako kuchagua.

Baada ya kuchukua futari yangu hapo sasa nakwenda kwenye lile duka la vyakula nikatafute vinywaji.

Rafiki yangu Mturuki kafunga tasbih mkononi lakini hasemi Kiingereza hili nalijua toka nilipofika dukani kwake siku ya kwanza.

Nikampa ishara kuwa nataka vinywaji.

Nikaelekezwa kwenye jokufu nadhifu lililosheheni kila aina ya vinywaji linamependeza ukiangalia kwa nje.

Kufungua nikapambana na kila aina ya ulevi na kila aina ya juisi.
Nikajiambia kheri nusu shari kuliko shari kamili.

Harare nililitewa nyama ya nguruwe kama futari.
Hizi chupa za juice kuwa pamoja na chupa za ulevi jambo jepesi sana.

Ukishangaa ya Mussa utaona ya Firauni.

Mwezi wa Ramadhani niko ndani ya ndege Egypt Air kutokea Berlin narudi Dar es Salaam ndege inaelekea Cairo ''transit,'' kisha Dar es Salaam.

Wahudumu wanataka kuwajua abiria waliokuwa katika saum kabla ya kutoa vinywaji na chakula.

Tumetua Cairo Maghrib wakati wa kufungua.
Uwanja umejaa Waislam wako transit wanaelekea Makka kufanya Umra.

Viwanja vyote vya ndege duniani siku hizi vina msala yaani sehemu maalum ya kusalia wapita njia.

Baada ya kufungua na kuingia restaurant kutafuta futari nakutana na FM Station za Cairo zinapiga muziki utadhani mwezi wa kula mchana.

Madhari ile hakika ilikuwa tofauti na ihram nyeupe zilizojaa mle ndani za waumini waliokuwa wanakwenda Makka kufanya Umra.

Hakika kusafiri ni elimu tosha.

Nimefananisha hali hii na siku nilipotua Tehran na Emirates nyakati za alfajir.

Nilichokisia uwanja wa ndege ni Qur'an ikisomwa.

Picha: Rovuma Hotel Maputo, 1990
Berlin 2011
Tehran na Watangazaji wa Radio Tehran 2006

1710622200164.png

1710622243227.png

1710622273128.png

 
Back
Top Bottom