Kusindikikiza mtu airport tu ndio wawekwe kwenye kumbukumbu za chama?
Amakweli maajabu hayaishi duniani
Mikocheni...
Umeuliza swali zuri kuwa kumsindikiza
Baba wa Taifa uwanja wa ndege ndiyo
wawe kwenye kumbukumbu za Chama?
Hakuna wa kukulaumu kwa sababu wewe hao wote hujui michango yao kwa
Baba wa Taifa binafsi, kwa TANU na harakati za kupigani uhuru.
Nitakueleza kwa mukhtasari tu na nitajaribu kukuwekea na links ili usome
zaidi na uelimike katika historia ya kupigania uhuru.
Katika picha juu ya hao akina mama wa kwanza kulia ni
Bi. Tatu bint Mzee
yeye ni katika akina mama wa kwanza kuingia TANU na kuitangaza nyumba
kwa nyumba na alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU mwaka wa
1955 na alikuwapo katika mkutano wa kujadili kujiuzulu
Mwalimu Nyerere
kazi ili ajishughulishe na TANU.
Mkutano huu ulifanyika nyumbani kwa
Clement Mohamed Mtamila Mtaa
wa Kipata na Sikukuu.
Mwenyekiti wa TANU (miaka ile TANU ilikuwa na Rais na Mwenyekiti).
Bi. Titi Mohamed naamini unaijua historia yake.
Aliyeko kulia wa kwanza kwenye picha ni
Bi. Chiku bint Said Kikusa au
Mama Sakina kama wengi walivyomwita.
Bi. Chiku yeye ni katika jamaa zake
Abdul Sykes na walimjua
Mwalimu
Nyerere kipindi kile alipojuana na
Abdul mwaka wa 1952 na alikuwa shoga
mkubwa wa
Mama Maria Nyerere na yeye ndiye aliyewahimiza wanawake
wa Dar es Salaam kujiunga na TANU na kushiriki katika mikutano ili mikutano
ile ishamiri na kunawiri.
Huyu alikuwa mke wa
Shariff Abdallah Attas.
Nani
Shariff Abdallah Attas?
Shariff Abdallah alikuwa mwanamji na katika watu wa kwanza kufahamiana
na
Nyerere pale sokoni Kariakoo alikokuwa akifanyakazi kama Mkusanyi
Ushuru wa Nafaka chini ya ofisi ya Market Master,
Abdul Sykes.
Hawa watu ndiyo waliomjengea
Baba wa Taifa msingi wa kufahamika na
kukubalika Dar es Salaam.
Shariff Abdallah Attas alikuwa mkubwa kwa umri kumzidi
Abdul Sykes
na
Abdul alimheshimu sana.
Kuna habari wamenieleza wajukuu wa
Bi. Chiku kuwa
Mwalimu katika
safari ile ya UNO aliondokea nyumbani kwa
Shariff Attas na
Bi. Chiku
Mtaa wa Mchikichi na New Street kuelekea Uwanja wa Ndege kwa ajili
ya kufanya dua kabla ya safari lakini nimeshindwa kupata uthibitisho
huru wa hili.
Itoshe tu kuwa
Bi. Chiku Kisusa alikuwapo katika msafara wa kumsindikiza
Baba wa Taifa katika safari hii muhimu sana katika historia ya
Mwalimu na
katika historia ya TANU.
Mwalimu aliporudi UNO mjukuu wa
Bi. Chiku, Jamila ndiye aliyemvisha
Baba
wa Taifa shada la maua.
Tuje kwenye picha hiyo ya chini kuna
Rashid Sisso huyu alikuwa bingwa wa
propaganda wa TANU akisimama nyuma ya
Nyerere katika mikutano yote ya
hadhara.
Robert Makange mmoja wa waandishi wa gazeti la TANU yeye na
Rashid
Kheri Bagdelleh.
Iddi Faizi Mafungo alikuwa Mwekahazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya na
ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya UNO.
Iddi Faizi alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo Hall mwezi
Agosti, 1955 mkutano ambao haukuzidi watu 20.
Kadi yake ya TANU na nduguye
Iddi Tosiri zinaongozana ni no. 24 na 25.
Hawa ndiyo waliomtambulisha
Nyerere kwa kaka yao
Sheikh Mohamed Ramia
wa Bagamoyo na TANU ikapata nguzo kubwa huko.
Yuko
Zubeir Mtemvu historia yake inafahamika.
Tusimame hapa ingawa yako mengi ya kueleza