Sun...
Unapotaka kuzungumza kitu ni bora kwanza ukakijua kwani ikiwa utajiandikia tu
huku somo lenyewe hulijui unajiweka wazi kwa watu kukulaumu.
The Torch on Kilimanjaro nimueleza
Mwalimu Julius Nyerere peke yake huwezi
kumkuta
Abdul Sykes.
Lakini nina wajibu wa kukufahamisha kuwa ikiwa ni historia ya uhuru wa Tanganyika
na TANU au historia ya Nyerere mwenyewe ni tabu sana tena sana kuwakwepa
Sykes brothers.
Chuo Cha Kivukono katika kitabu chao, Historia ya Chama Cha TANU wamejaribu na
matokeo yake ndiyo haya wewe unawataja hapa kwa nini wanatajwa sana.
Sasa nakuja katika historia ya TANU na kudai uhuru.
Nakuomba usome hapo chini kutoka kitabu cha
Abdul Sykes:
''...mkutano huo wa muhimu katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ulifanyika miezi sita tu baada ya Nyerere kuchukua ofisi kama rais wa TAA. Tarehe 29 Oktoba, ujumbe wa TAA ukiwa na Mmanyema na mtunga mashairi, kiongozi mashuhuri kutoka Jimbo la Ziwa, Abdu Kandoro, Chifu Patrick Kunambi kutoka Morogoro, Jimbo la Mashariki, Japhet Kirilo, Joseph Kimalando, John Rupia na Julius Nyerere, walikutana katika Government House kujadili ile sekula ya serikali na Gavana Edward Twining...''
''...jibu la Twining kwa ujumbe wa TAA juu ya ile sekulla lilitabiriwa na hoja ya kupinga iliyotayarishwa wajumbe walipokutana katika makao makuu ya TAA kupanga maneno ya kusema mbele ya Gavana. Kunambi aliyekuwa msemaji wa ule ujumbe wa TAA alimwambia Twining; ‘’Je, unajua kitakachotokea bwana mkubwa, ikiwa, kwa mfano serikali itapitisha sheria kuwapiga marufuku madereva wote wenye ujuzi wasiendeshe magari ikawataka wasalimishe leseni zao za udereva na kuyaacha magari yao yaendeshwe na madereva wasio na ujuzi?''
''...joto la siasa lilikuwa katika kiwango kama hiki wakati wajumbe kumi na saba wa TAA kutoka kwenye matawi majimboni na makao makuu walipokutana mjini Dar es Salaam tarehe 7 Julai, 1954, kujadili katiba mpya ya chama kipya cha siasa - TANU. Jimbo la Mashariki ambalo lilikuwa na wajumbe wengi kushinda yote liliwakilishwa na, ndugu wawili Abulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Patrick Kunambi, Kasella Bantu, John Rupia, Julius Nyerere na C. O. Milinga; Jimbo la Kaskazini liliwakilishwa na na Joseph Kimalando na Japhet Kirilo; Jimbo la Ziwa liliwakilishwa na Abubakar Kilanga, L. M. Makaranga.''