The Giantist
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 214
- 86
Na: Giantist McWenceslaus
20/09/2020
Dodoma
www.ccmmpya.org
Habari za muda ndugu wanabodi wenzangu. Ikiwa tumebakiwa na siku 38 za kutimiza ule wajibu wetu na haki yetu ya kikatiba wa kwenda kumchagua Rais, wabunge na madiwani ili waweze kudumu katika serikali kwa miaka mitano kwa kusudi la kuijenga nchi yetu na kuboresha maisha ya watanzania wa sasa na wa vizazi vya baadaye. Na ikiwa tutaweza kutimiza wajibu wetu huo, ni dhahiri kuwa tutakuwa tumewajibika kwa serikali yetu kwanza serikali yetu kwa kuiweka madarakani na kisha serikali yetu hiyo itawajibika kwetu sisi katika kutuletea huduma nzuri za jamii ikiwa ni Afya, Elimu na Maji ambazo ni kitovu cha maendeleo ya watu. Bila shaka jambo hilo linafahamika kwa watanzania wengi sana.
Narudia kusema kuwa KUMCHAGUA MAGUFULI NA CCM NI KUONDOA UKAME TANZANIA. Jambo hili ni la kweli, kwanini tunasema hivyo... Ni ukweli usiopingika kuwa, kazi aliyoifanya Dkt. John Pombe Magufuli chini ya uongozi wa ilani ya CCM ya 2015/2020. Serikali ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha Huduma ya Maji kwa wananchi inakuwa ni ya uhakika na yenye kuwatoshekeza kwa matumizi ya nyumbani, shambani umwagiliaji pamoja na shughuli za viwandani. Na kwamba hata yale maeneo ambayo ni ya ukame, basi watu wake wataweza kupata huduma ya maji yaliyo safi na salama kwa matumizi ya Binadamu.
Niliwahi kusema hapa, kwamba "KWANINI TUICHAGUE CCM na MAGUFULI KWA MIAKA MITANO TENA" nilitoa sababu kadhaa ikiwa ni ushahidi kwa mambo mazuri ambayo Rais Dkt. John P. Magufuli na ilani ya CCM ilivyoweza kuwahudumia wananchi vema katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na utekelezaji mzuri wa mikakati mbalimbali na hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Sekta ya miundombinu ya ujenzi, Mawasiliano na usafirishaji. Madhumuni yao ilikuwa ni kuleta maendeleo kwa watanzania wote na kupunguza gepu la upatikanaji kwa huduma muhimu za jamii baina ya watanzania wengi wanyonge masikini na watanzania wachache matajiri.
Sasa leo nitazungumza nanyi kwa uchache kuwaambia ukweli na nia ya dhati ya ilani ya CCM ya uchaguzi wa 2020 na nia za dhati ya Rais Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI katika kuwahudumia wantanzania kwa miaka Mitano mengine mpaka 2025, katika sekta ya maji na katika uhifadhi wa mazingira ndani ya nchi. Na nia ya dhati hiyo ya CCM na ya Rais Dkt. JPM inadhirishwa na yale yaliyotekelezwa katika sekta ya maji kwa miaka Mitano ya mwanzo 2015-2020. Yafuatayo ni kazi ambazo CCM na Dkt. JPM wamezitekeleza kwa miaka Mitano na kwa sababu hiyo bado wanayo nia na sababu ya kwenda kuyaendeleza kwa miaka miatano mengine.
Maji ni uhai, vilevile maji ni moja ya nyenzo muhimu katika kuboresha uchumi wa watu na wa nchi. Jamii yoyote ile ili iwe na uhai katika sekta zingine zote basi haina budi kuipa kipaumbele sekta hii ya maji, ili kwamba jamii ikishaondokana na UKAME Basi inakuwa rahisi kwa wananchi kuweza kuboresha hali ya uchumi wa jamii.
Tanzania imebarikiwa kuwa moja ya nchi kati ya nchi nyingi zenye hazina kubwa ya maji, ambapo inakadiriwa kuwepo kwa hazina ya mita za ujazo wa maji wa zaidi ya Bilioni 150, hii ni sawa na wastani wa mita za ujazo wa 2250 kwa kila mtu kwa mwaka. Hiyo pekee haitoshi, ni kwamba Tanzania ni nchi ya maziwa Makuu matatu, ikiwa ni ziwa la Viktoria, ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa. Hii ina maana kuwa ukiachana na hazina ya maji iliyopo kwenye vyanzo vya ndani, pia tumebarikiwa kuwa vyanzo vya nje vya maji katika mziwa yetu Makuu. Kutokana na rekodi hiyo ni dhahiri kuwa Tanzania inahitaji chama makini na viongozi makini katika kuhakikisha kuwa watu wote wanayapata Maji hayo.
Kwa kutambua hazina hizo za maji, serikali ya Tanzania kwa maelekezo ya ilani ya CCM ya 2015/2020 chini ya uongozi wa Rais Dkt. John P. Magufuli, iliamua kuja na miradi mikubwa yenye lengo la kuongeza upatikanaji wa maji lakini pia kuondoa kero zilizokuwa zikiwapata wanawake wakati wa kutafuta maji. Wote tunafahamu uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo mengi nchini, na kwamba ndio uliopelekea madhira ya unyanyasaji kwa wanawake na kwa wasichana ambapo ilichangia katika kusababisha mimba za utotoni kwa mabinti wanafunzi n.k.
Na kwa kuwa serikali yetu ilifahamu madhira hayo, ikaonelea kuongeza bajeti ya fedha katika serikali kupitia wizara ya maji na umwagiliaji katika kushughulika na matatizo hayo, tangu Rais Dkt. John P. Magufuli aingie madarakani ameweza kupandisha bajeti ya wizara kufikia wastani wa zaidi ya shilingi Bilioni 500. Hii Ina maana kwamba serikali imeazimia kwa dhati kabisa kuondoa kero ya maji kwa watanzania.
Maendeleo ya sekta ya maji yapo wazi na kwamba imejidhihirisha yenyewe kwa watanzania. Na ukweli huu ni kwa sababu hakuna namna ambayo binadamu anaweza kutengana na maji. Binadamu ni Maji! Serikali ya CCM imeweza kupandisha bajeti ambayo imeweza kutekeleza jumla ya miradi ya maji 1423 mijini pamoja na vijiji ambapo miradi 1268 ni ya vijijini na miradi 155 ni ya mijini. Hata hivyo serikali pia imeendelea na kutekeleza miradi mikubwa ya kusambaza maji katika vijiji zaidi ya 200 na miji zaidi ya 70, kutika katika maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa, ambapo ili serikali iweze kutekeleza miradi hiyo imekuwa ikikarabati na kujenga miundombinu ya maji pamoja na kuchimba visima na kujenga mabwawa katika maeneo ambapo hazina ya maji ya chini inaweza ikavunwa kwa matumizi ya binadamu. Na kwa hakika miradi yote hiyo inatekelezwa kwa fedha za watanzania wenyewe.
Nitajitahidi kueleza kwa ufupi ili nisithubutu kuwachosha kwa maelezo mengi sana. Na kama nilivyotangulia kusema kuwa serikali ya CCM kwa miaka Mitano imeazimia kuondoa kero ya maji kwa wananchi kwa kuwaletea maji Safi, salama na yenye kutosheleza lakini pia kuwezesha kukua kwa sekta ya viwanda nchi ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mazingira. Katika kuhakikisha jambo hilo linatimia, Tanzania imeweza kupata mkopo nafuu kutoka serikali ya India wa shilingi trilioni 1.2 ili kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji katika miji zaidi ya 20 hapa nchini. Na mkopo huo utalipwa na sisi watanzania wenyewe. Lakini lengo ni kuharakisha idadi ya watanzania wanaopata huduma ya maji ya uhakika na yaliyosalama inaongezeka.
Kwa hiyo katika kutekeleza miradi hiyo ndani ya miaka Mitano ya kwanza ya Rais Dkt. John P. Magufuli ameweza kupandisha idadi ya watanzania waliokuwa wakipata huduma ya maji Safi na salama kutoka 47% mwaka 2015 kwa upande wa vijijini mpaka 75% mwaka huu 2020: na kutoka 74% na kufikia 85% kwa upande wa mjini. Hakika haya ni mafanikio makubwa sana. Kwa makadirio hayo CCM imebakiwa na 25% ya idadi ya watu vijijini ili kuondoa kero ya maji kabisa kabisa na 15% idadi ya watu mijini... Na hiyo itawezekana ikiwa tuirudisha tena ilani ya CCM ya 2020-2025 na Rais Dkt. JOHN P. MAGUFULI kwa miaka Mitano mengine ili kuweza kuielekeza serikali kuiendeleza miradi hiyo kwa miaka Mitano mpaka mwaka 2025.
#chaguaCCM
#chaguaMAGUFULI
#ilikuondoaUKAME
Sauti ya Mdodomia