Uchaguzi 2020 Kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais ni kuikabidhi Tanzania kwa Mabeberu. Tusifanye kosa twende na John Pombe Magufuli

mwananyaso

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
2,995
Reaction score
3,401
Lissu hafai kuwa Rais wa nchi hii, Ubunge ndio ilikuwa level yake ya juu na ya mwisho.

Kumbukeni alikuwa kwenye matibabu huko ughaibuni mara alipopata nafuu, kazi yake ilikuwa kuzungumza mambo ya hovyo sana, kutaka nchi iwekewe vikwazo, kukubali kuruhusu ndoa za jinsia moja, pindi akiwa mtawala , na ifahamike ni kinyume na mila na desturi zetu nchini ,alifanya mambo ya fedheha sana.

Wazungu walimsikiliza wakaona huyu ni bogus kabisa, ndio maana pamoja na kelele zake na maombi yake hayakuwa na impact yoyote.

Mtaji aliobakia nao kwa sasa ni kupata kura za huruma kwa risasi zilizompata

Pia system haiwezi kukabidhi nchi kwa mtu anayetetea mapenzi ya jinsia moja na msaliti kwa taifa lake,si mnakumbuka vitisho vyake na MIGA?,yako wapi?,tumeunda kampuni ya Twiga minerals Tanzania kwa ubia ambao unalinufaisha taifa, kongole Rais Magufuli.

Namuonea huruma sana, kwa maana baada ya uchaguzi atapotea kwenye ulingo wa siasa, kiki hazitakuwepo , Bunge ndio lilikuwa linampa kiki, miaka mitano sio mchezo kukaa benchi
 
Hata yule hafai ni nguvu tu anazotumia lakini hata udiwani hatakikani apewe.
 
Umelalamika tu.

Kama Nyerere aliongoza nchi mwl kijana 39 yrs. Na alionyesha mafanikio, Mwinyi na diploma ya ualimu lakini alitupa ruksa, Mkapa toka uandishi mpaka Rais alieacha impact . Kikwete na democracy ya Kiswahili lakini alimaliza salama. Na sasa tunae Mwl mwingine tena wa sayansi lakini hajashindwa.

Ndiyo aje ashindwe advocate msomi anayetaka nchi iongozwe kwa sheria na katiba ?!

Lissu yuko vizuri kuliko team ilioko uwanjani saa hii. Hata wewe unajua. Labda figisu tu. Na ndiyo keshasema hatamuachia Mungu . Mnalo
 
Kwa kura za mitandaoni zenye fake IDs za kutosha?
Haya mkuu
Tumeshawazoea maneno yenu. Wa mitandaoni ndo tulijitokeza kwa maelfu kumpokea airport tarehe 27 na kama message nauhakika mliipata hakika
 
Mtoa mada kuwa serious, hivi unaanzaje kufikiria kuwa Watanzania watamchagua yule!?

Achana na mambo mengine yote, gwaride atakaguaje!?

Hivyo hii mada yako ingepaswa kuwa, Watanzania tusifanye makosa ya kumchagua JPM kwa kura chini ya asilimia 80 na badala yake JPM ashinde kwa kura asilimia 90 na zaidi. Mada yako ilipaswa kuwa hivyo.
 
Wasukuma!!
 
Mmeanza kuweweseka na bado.

Msiyempenda kaja.

Nyimbo za mabeberu zimeshafubaaa.
o
 
CCM tulieni demokrasia ifanyike nchi tumekosa demokrasia kwa miaka mingi. Yule tishio la jiwe amerudi na watanzania wanamkubali kuliko hapo mwanzo, hii ni mipango ya Mungu, jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni. Siasa anazofanya magu ni za kibabe na kidikteta kamwe hazikubaliki, tupo na Tundu Antipas Lissu mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…