Kumekucha: Abdalah Bulembo kuishtaki TFF ya Karia mahakamani

Kumekucha: Abdalah Bulembo kuishtaki TFF ya Karia mahakamani

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Bulembo,mzee mustaafu mwenye hekima zake ameapa kupeleka shauli mahakamani kuishtaki TFF ili iondoe kipengele cha lazima uwe na elimu ya Shahada ama degree ndipo uruhusiwe kugombea Urais na u makamo wa Rais wa TFF.

"...kipengere hicho kinakiuka katiba na miongozo ya wenye mpira Duniani na Afrika yaani FIFA na CAF kwa sababu katiba ya FIFA na CAF haina kipengere hicho.Ajabu hapa kwetu kuna kakisiwa kametengenezwa ili kutowapa mwaya hasa vijana wetu waliocheza mpira kuwa Viongozi wa chama chetu cha soka." Alinukuliwa Bulembo.

"...siyo nasema hivyo eti kwa sababu nataka kugombea la hasha mimi ni mustaafu lakini nawasema kina Lunyamila na wenzake ambao wao waliocheza mpira ajabu kanuni zetu zinawatenga wao kuwa Viongozi wa baadae wa mpira wetu." Amesema Bulembo.

"...nimewasilisha malalamiko yangu Wizara ya michezo,baraza la michezo na TFF pia na wote wameshaipokea.Sasa kabla ya uchaguzi ujao wa TFF ihakikishe inabadiri kipengere hicho vinginevyo nawapelekea mahakamani." Abdallah kasema.

My take: Hongera sana mzee mustaafu Bulembo kwa nia yako safi yenye kusudi chanya ya kuliokoa soka letu.

Pamoja na uanasimba wako angalau umethubutu kuisimamia haki ya mpira.
 
Namheshimu sana mzee wetu, mh.Comrade Alhaj Abdallah Bulembo....

Heshima yangu kwake iko kuanzia nikiwa kijana mdogo kule K/nyama naye akiwa mh.Diwani na mtu wa karibu sana kwa wapiga kura wake...

Heshima yangu inayofuata ni pale nilipomuona akiifanya KAZI YENYE KUNG'ARA katika kumnadi kipenzi chetu Hayati JOHN POMBE J.MAGUFULI majukwaani na kuratibu mchakato wa KAMPENI ZILE CCM iliyoshinda kwa KISHINDO chengine....

Laa Upande wa pili ,simuungi mkono hata kidogo juu ya HOJA yake ya kutaka WASIO NA SHAHADA kupewa nafasi ya kugombea URAIS na UMAKAMU RAIS WA TFF kwa hoja zifuatazo :

1)Kuishia madarasa ya CHINI si kigezo cha kushindwa kujiendeleza hasa katika dunia hii ya sasa.
Yuko mzee mmoja mtu mzima sana wa WEKUNDU WA MSIMBAZI ambaye ALIJIENDELEZA kutoka "madarasa yake ya ngumbaru" mpaka KOZI YA QT ya miaka miwili na akamaliza KIDATO CHA 4...je kinachowashinda kujiendeleza kusoma hao vijana wastaafu asemao ni kipi ?!!!

2)Mfano mwingine japo watu hawatoupenda kwa kuwa ni wa "ulaya" ila nami sitouacha....TONY ADAMS nahodha nguli wa zamani "kilabu cha Arsenal" cha nchini Uingereza ,alipostaafu alipata kujiendeleza ELIMU YA CHUO KIKUU NA KUCHUKUA SHAHADA YAKE YA SHERIA....

Kwa hiyo ni kuwa wachezaji wetu wastaafu wanakosa tu malengo ya kujiendeleza huku wakiwa na SABABU LUKUKI ambazo nadhani si mujarabu sana katika MAPAMBANO YA DUNIA HII YENYE CHANGAMOTO mpya kila UCHAO....

Hivi mchezaji kama THADEO LWANGA na BERNARD MORRISON wa SSC wangekuwa watanzania na pale wakistaafu wasingekuwa na SIFA YA KUGOMBEA NAFASI KUBWA ZA TFF?!!!!!

3)Kiukweli hapo TFF ni vyema kipengele hicho cha "usomi" kikaendelea kwani soka la kisasa na dunia ya kisasa huwezi KUIACHA ELIMU NYUMA YA MGONGO.

Namheshimu sana El Comandante Kiongozi wangu wa CCM ,Mzee wetu Comrade Alhaji Abdallah Bulembo ila kwa hili ninamsihi asiende MAHAKAMANI kwani soka na Mambo ya mahakama ndio "alarming point" ya kuweza KUFUNGIWA KIMATAIFA japo mahakama ni sehemu ya KUTAFUTA haki na ambako MTANZANIA hazuiwi kwenda huko!!!

Wasalaam!

#KaziIendelee
 
Hadi sasa nauliza.... Mashindano ya kimataifa na ya Afrika mashariki Taifa Stars ina vikombe/ubingwa mara ngapi..????!!??????

Kweli tunaona vijana wanacheza Soka,

tunafuatilia Ligi kuu... tunapenda mpira wa miguu... ila matokeo vipi????
 
Hadi sasa nauliza.... Mashindano ya kimataifa na ya Afrika mashariki Taifa Stars ina vikombe/ubingwa mara ngapi..????!!??????

Kweli tunaona vijana wanacheza Soka,

tunafuatilia Ligi kuu... tunapenda mpira wa miguu... ila matokeo vipi????
Ukhty wangu mwalimu wa kozi za lugha za kigeni nduguyo niseme tu TUNAPIGA "MAKTAIM"....

Soka letu limejaa "pang'ang'a" nyingi zaidi ya utekelezaji kuntu....

Bado hamu ya kupata hivyo vikombe iko juu sana...ila sasa...ila Sasa....hayaaa TUTAFIKA insha Allahu Aaamin!!

#KaziIendelee
 
Mkuu Hicho kipengere cha Elimu alikiweka Karia?
halafu mbona Thaddaeus Lwanga ni Engineer? kipengele kiliwekwa siku nyingi, kwa nini hakumshauri Lunya kusoma hata QT tu?
ina maana wale waliokusanywa na Kanali Kipingu pale Makongo walikuwa wanakula na kulala tu ili wachezee Serengeti boys na si kuingia darasani!!!! Fikiri kabla ya kusema.
 
Nashangaa sana kumuita huyu Mzee eti ana busara na hekima ili hali ni mtu mmoja mzurumaji wa mali za watu masikini; akitumia nafasi zake ndani ya CCM!

Pale Mbezi beach amemdhulumu nyumba ya mjane mmoja tena muhaya mwenzie na kuivunja ile nyumba na kumuacha yule mama analala nje na watoto wake kwa Mwaka wa nne sasa!!!

Hiyo hoja anayojenga ni kujitafutia ulaji tu!
 
Duu mimi nikidhani unataka kumshitaki kwa kusababisha hasara na usumbufu kwa wananchi baada ya mechi ya simba n yanga kubadikishwa muda bila sababu za maana kutokewa. Tanzania kuna vyuo vikuu zaidi ya 50, kwanini tuwe na kiongozi ambae hana degree?
 
Nadhani mzee Bulembo hakushauriwa vyema kwenye hili......ni vyema akarudi na kujitafakari.......wakati watu wanaopambana soka letu liendeshwe kisasa kwa viongozi wenye elimu yeye tena anataka kuturudisha nyuma.........
.....
 
nilisikitika sana Dalali alipokataliwa kugombea kwa kigezo cha elimu, akiwa mwenyekiti alianzisha Simba day, alinunua uwanja wa Bunju pia aliwapiga utopolo 5 bila lakini vyote havikuangaliwa bali elimu yake wakawapitisha kina Nkamia ambao pamoja na elimu yao hawana chochte
 
Nadhani mzee Bulembo hakushauriwa vyema kwenye hili......ni vyema akarudi na kujitafakari.......wakati watu wanaopambana soka letu liendeshwe kisasa kwa viongozi wenye elimu yeye tena anataka kuturudisha nyuma.........
.....
Anataka turudi enzi za akina ndolanga, hassan dyamwale
 
Nadhani kiongozi wa mpira inatakiwa awe na PhD.
Wale darasa la saba wabaki kushangilia tu
 
Back
Top Bottom