Kumekucha Dar es Salaam, ndani ya Landmark Hotel

Kumekucha Dar es Salaam, ndani ya Landmark Hotel

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
961
Reaction score
533
Ni tarehe 20/09/2014 ndani ya Landmark Hotel, ni semina ya aina yake kuwahi kufanyika. Nitakuwemo katika wale watakao toa mada siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wafugaji na wanaohitaji kuanza kufuga nk. Karibu tukutane tuonyeshane utajiri uliojificha katika ufugaji wa kuku, hakuna haja ya kulalamika. Anza sasa kufuga kuku unufaike Kiuchumi.

Ni semina ya aina yake kwasababu mambo mengi yatahusika siku hiyo kama ambavyo yamebainishwa kwenye hilo tangazo hapo chini.

Tutakuwa na watu wa mabank ambao bank zao zinatoa mikopo kwa wafugaji, tutakuwa na mameneja wa Hotels mbalimbali, supermarkets pamoja na wamiliki wa bars kubwa, hawa ni wanunuzi wa mazao ya kuku.Tutakuwa pia na wazalishaji wa vifaranga, watengenezaji wa vyakula vya kuu, Pia kutakuwa na maonyesho siku hiyo. Mada mbalimbali zitatolewa siku hiyo na wataalam waliobobea katika tasnia ya kuku

Kwa hakika Siyo siku ya kukosa. Karibuni nyote.

LANDMARK HOTEL.jpg
 
Wazo zuri. Tutakuwa pamoja
 
Msitusahau wengine tupo mbali na ratiba zinabana.
Natumai mtatupia kwa utube kitakachojili.
 
Hii Semina baada ya Dar es salaam itaenda Songea kisha mwanza hivyo wakazi wa maeneo hayo muanze kujiandaa kwa elimu na mawazo ya kimaendeleo
 
Mkuu na sisi wa huku mji kasoro bahari huku kwa kina mkude simba tutasubiri mpaka ujio wa nani? matayo mbatizaji au say'dina abubaakar??
 
Please count me in
Mheshimiwa Bluetooth,
Kwenye hilo tangazo hapo juu, kwa chini kuna namba za simu za mratibu wa semina hiyo madam Sekela Ms wa shirika la Communication Solution (CoSo), ndiyo anayesajili watu wanaohitaji kushiriki katika semina hiyo, tafadhali naomba umpigie simu ili aweze kuku count na kukuingiza katika orodha ya watakaoshiriki siku hiyo.
 
Mkuu na sisi wa huku mji kasoro bahari huku kwa kina mkude simba tutasubiri mpaka ujio wa nani? matayo mbatizaji au say'dina abubaakar??

Bwana Kisima,
Morogoro na dsm sio mbali, kama una nia ya kushiri unaweza kufanya hivyo.
 
Mkuu kama hutojali nitajie hizo benki zinazotoa mikopo nijue kama zinahuduma hadi huku upcountry.
 
Back
Top Bottom