Diwani Mtarajiwa
Member
- Feb 3, 2010
- 19
- 0
Kinyang'anyilo cha uchaguzi wa kura za maoni mwaka huu katika jimbo la Nzega kimeanza kwa vibweka baada ya mbunge wa jimbo anayemalizia muda wake Lucas L selelii kuzomewa mwanzo hadi mwisho alipopewa nafasi ya kujieleza huku wananchi wakimzomea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mkutano huku wakipaza sauti Asulubiwe! Asulubiwe! hatumtaki hali ilyopelekea hatari ya mkutano kuharibika . kibaya zaidi ni pale alipopanda Husen Bashe yeye alishangiliwa kiasi cha kushindwa kujieleza kwani kelele za wananchi zilikuwa kubwa mno na baadae wananchi wakakumbusha enzi za mrema kwa kulisukuma gari la Bashe hadi pale vyombo vya usalama vilipoingilia kati kwa kuuzuia umati huo wa watu