Elections 2010 Kumekucha Nzega! Selelii azomewa mwanzo mwisho!


Na vipi kama hao washangiliaji wamekodiwa kwa kazi hiyo? umefuatilia, Je hao ni wapiga Kura kweli? mbona wanakodi Baiskeli kufuatilia mikutano? nina wasiwasi. Fisadis at work
 
Heshima kwako Diwani,

Inawezakana unatoa taharifa za kweli lakini napata shaka kidogo baada ya kufuatilia post zako za nyuma inaonekana unapenda ushabiki kitu amabacho si kizuri ndani ya jamvi la JF.Uzuri wa hili jamvi ukileta ushabiki utajulikana tu utafanyeje pengine tungepata taarifa kutoka chanzo kingine ingeweza kusaidia sana.
 

kwa sababu wewe ni mpambe wa bashi kwa hiyo habari yako inachukuliwa kuwa ni ya kipambe tu.
 
Heshima mbele wakuu!
inawezekana kabisa mimi ni shabiki wa Bashe, inawezekana kabisa nimetumwa na RA/EL and what ever haki yangu ya kushabikia mtu au kitu haipokonywi na mtu au kitu chochote kama vile watu ambao wangependa leo CCM isambaratike na ife kabisa wakati wengine tukikesha tukisali kuomba CCM itawale milele!
 
Huyu Bashe si ni pandikizi la fisadi Rostum? Vipi watu wa Nzega wasilijue hili?
 
Kwa hiyo kazi yako ni kumpamba huyo jamaa huku JF?
 
Diwani,
Hivi Bashe atakaposhindwa kupata Ubunge utakuja kwa mbwembwe tena kutujulisha?
 
Sawa kabisa, ila nakushauri ushabikie kwa kumsifu unayempenda, siyo kwa kumsemea uongo au kuudanganya uma juu unayemchukia!
We sema tu huyo jamaa yako ni kidume cha mbegu, au mwanaume wa shoka kama wasemavyo akina Sophia Simba tutakuelewa!
 
Hao wananchi wa Nzega kama kweli wamemzomea mpiganaji Selelii hawajui watendalo.
 
Mimi nataka hawa wabunge wa SISI EMU wote washindwe na hao watakaoshinda kura za maoni washindwe katka uchaguzi, i hate CCM!!!
 
huyu jamaa hana uhakika kwani mimi nipo nzega na hali hiyo haipo acheni uongo

we umetoka wapi?
Junior Member Join Date Sat Jun 2010
Posts 3
Thanks : 0
Thanked 2 Times in 1 Po
 
Huyu Bashe si ni pandikizi la fisadi Rostum? Vipi watu wa Nzega wasilijue hili?

umaskini wenu ndio angamizo lenu....huna hela huna sauti katika nji hii..kelele zitapigwa na hao mnaoita mafisadi watapeta kama kawa
 
Wewe ndugu usinilazimishe nikukabili wewe binafsi kwani ninawasiwasi na uwezo wako wa kueleza haya. Jifunze namna njema ya kutoa propaganda. Ninachokiona kwako unashindwa kueleza maeneo ambayo Bashe hakubaliki unajihalibia bure hatra hiyo kazi uliyo pewa itakushinda na watakuona haufa hiza pesa za richmond Nzega hazitafua dafu tupo tayari kum pa kura Dr. Kigwangala kuliko kumpa kura mtu asiyeaaminika. Nzega inawenyewe na chuki yenu kwa Selelii inazidi kumuongezea umaarufu. Njoo hapa Nata, lussu ambapo makao makuu nyake ni Mwaluzwilo, nenda Wel;a, Mbogwe , Mwanhala kote huko richmond inafahamika. hampati kitu zaidi ya kum uongezea umaarufu selelii. bado unamashaka na mimi niliye nzega vijijini?
 
umaskini wenu ndio angamizo lenu....huna hela huna sauti katika nji hii..kelele zitapigwa na hao mnaoita mafisadi watapeta kama kawa

Inasikitisha, lakini ndiyo ukweli. Mafisadi wameshika nchi, na wanamiliki almost everything in this country. Everybody need to stand-up and be counted; NOW!!
 

Diwani naomba nikuulize swali moja, Seleli kazomewa kwa kosa gani hasa alilolifanya? na Bashe kashangiliwa sana kwa kipi alichowafanyia wananchi wa Nzega? Maoni yangu kwako, next time naomba utuchukulie clips ya hivyo vitendo kwenye video au hata kwenye simu yako unayotumia kukutumia hizi information.
 
PHP:

Asalaam aleikum waungwana wote. Mimi nakiri ugeni katika forum hii mahiri.
Naamini anayotujuza Diwani kuwa yanatokea na yataendelea kutokea.
Swali kwetu sote ni kuwa yanatokea kwa sababu wanaNzega hawamtaki Selelii au kwa kuwa watu fulani wanamwogopa sana Selelii hivyo hawataki arudi Bungeni?
Kwa nini sisi Watanzania tunakubali wachuuzi wa chumvi na pembe za ng'ombe watupangie wabunge wetu?
Watanzania tunajua kuwa huo unaoitwa utajiri uliokithiri wa hao wanaowapinga wazalendo kama Selelii, wamepata utajiri kupitia jasho la Watanzania kwa njia za kifisadi?
Mwana Forum Diwani anaandika kwa namna ya kushangilia kuwa Selelii kazomewa; hivi hata Watanzania wachache wenye angalau mwanga kidogo wa elimu wanaweza kushabikia kuzomewa kwa mpiganaji mahiri dhidi ya ufisadi?
Tanzania ni nchi tajiri sana. Kwa nini Watanzania tunaridhika kuendelea kuwa masikini huku tukishabikia utajiri wa mafisadi?
Wale tulio na mwanga kidogo tunao wajibu wa kuwaelimisha wale waliojinyima ili sisi tuelimike maana bila kujali mahali tuliposomea, mchango wa Watanzania masikini ni mkubwa sana kwetu sote.
Wana Nzega waelimishwe kuwa kuchagua vibaraka wa mafisadi kutawagharimu sana mbele ya safari
 
waache wafu wawaziki waffu wenzao kazi tanzania ipo kweli kweli.enyi wafanyakazi wana JF tuko wapi kuwaelimisha hawa wanaohongwa kanga na fulana nchi iteketee
 
BASHE ANAANGUKA KWA KISHINDO KWANI HAPA LUSSU YAANI9 MWALUZWILO WATU WANADAI NI BORA APITE KIGWANGALA Dr. kuliko huyu wa richmond
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…