Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Askari kulipua siri ya uchaguzi Zbar
na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SAKATA la kukwama mafao ya askari wastaafu wa vikozi vya SMZ, limechukua sura mpya, baada ya baadhi yao kutishia kufichua siri ya jinsi walivyotumika katika uchaguzi mkuu wa 2000 na 2005 Zanzibar.
Wakizungumza na Tanzania Daima jana, askari hao walisema wanatoa wiki mbili, mapandekezo ya mafao yao mapya, yawe yamezingatiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar, vinginevyo watamwaga siri hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, askari hao walisema kwa kuwa sheria iliyotumika kuandaa viwango vipya vya mafao yao ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi na kusainiwa na Rais wa Zanzibar, hakuna chombo kingine chenye uwezo wa kupinga maamuzi hayo.
Walisema Wizara ya Fedha na Uchumi, ilipaswa kugundua kasoro zinazojitokeza kabla ya muswada wa sheria kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi na kusainiwa na Rais wa Zanzibar, kama sheria.
Askari hao walisema wanashangazwa na mapendekezo hayo kuzuiliwa wakati miongoni mwa wajumbe wa tume hiyo ni watendaji wakuu Serikalini.
Hapa kinachoonekana hawathamini mchango wetu, tumetumika sana kwenye uchaguzi na tunajua mambo mengi, hiki ni choyo cha watendaji wa Wizara ya Fedha, alisema afisa mmoja mstaafu ambaye alifikia cheo cha juu katika kikosi cha KMKM.
Walisema inashangaza kuona watendaji wa Wizara ya Fedha, wamekuwa na kinyongo kulipa mafao yao wakati baadhi yao wameajiriwa hivi karibuni na wanamiliki mali nyingi, yakiwemo majumba na magari.
Walisema hivi sasa taratibu zimeshakamilika za kuzungumza na mwanasheria atakayesimamia kesi yao mahakamani.
Wiki iliyopita, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Hassan Haji Wambi, alisema mapendekezo ya mafao ya askari hao wastaafu yamekwama baada ya kutokea mgongano wa kisheria kati ya Sheria ya Tume ya Uajiri namba 7 ya mwaka 2007 na sheria ya fedha ya mwaka 2005.
Alisema sheria ya Wizara ya Fedha, inalazimisha kuwepo mashauriano kabla ya viwango vipya vya mafao kupangwa, ili kuepusha kuathiri bajeti kuu ya Serikali.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali imeamua kuwalipa askari wote viwango vya zamani, wakati suala hilo likiendelea kutafutiwa ufumbuzi na mamlaka husika.
Mafao ya askari hao wastaafu yamerekebishwa na kuongezwa kwa zaidi ya asilimia 50 ya viwango walivyokuwa wakipata zamani, lakini walilazimika kulipwa kwa viwango vya zamani baada ya kujitokeza hali hiyo.
Askari wa vikosi vya SMZ wamekuwa wakitajwa katika ripoti mbali mbali za uchaguzi kuwa ni miongoni mwa wanaoshiriki katika uchaguzi na kusababisha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa.
SOURCE: tANZANIA dAIMA