Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu nimesikia habari kwamba jana kulikuwa na vurugu mwz, eti kidogo mabomu yapigwe na dr.slaa ndiye ameepusha ghasia.magazeti hayafunguki humu na jf sioni chochote.nijuzeni tafadhali wenye hizo habari.
Ni kawmba wadau waliofika kumsikiliza dr.slaa waliamua kutumia nguvu zao kwa kusukuma gari alilokuwa amepanda dr.slaa kama mchango wao wa mafuta.Polisi kuona hivyo ndio wakawa wanatishia kuwapiga mabomu,ndipo dr. alipotumia busara zake kuwanyamazisha polisi.
Wakuu nimesikia habari kwamba jana kulikuwa na vurugu mwz, eti kidogo mabomu yapigwe na dr.slaa ndiye ameepusha ghasia.magazeti hayafunguki humu na jf sioni chochote.nijuzeni tafadhali wenye hizo habari.
Busara ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willibroad Slaa, juzi iliepusha shari mjini Mwanza, baada ya kuwataka polisi waliokuwa wamejiweka tayari kumwaga maji ya kuwasha na mabomu ya machozi dhidi ya wananchi, kuacha kufanya hivyo.
CHANZO: NIPASHE
Nidhani ni vyema vyama vya upinzani wajitahidi mno kuwa japo na mpiga picha na mwandishi wa mgombea urais ambao watakuwa wakisambaza taarifa na picha kwa kutumia blog, tovuti na hata email za vyombo vya habari mbalimbali maana habari zao na picha halisi ya mikutano yao huwa zinafichwa na kuminywa na mfumo CCM. Matokeo yake ni maswali kama haya kwa wanaotaka kupata ukweli.