Kumhudumia mgonjwa asiyejiweza kabisa

Kumhudumia mgonjwa asiyejiweza kabisa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Magonjwa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Yanaweza kuwa muendelezo wa magonjwa ya muda mrefu, ajali kama stroke au kugongwa na Gari. Inaweza kutokea kwa mume/mke, Baba/mama au mtoto wako. Si wengi wenye uwezo wa kulipa mtu mwenye taaluma na ujuzi wa kumtunza mgonjwa. Nimeamua kuandika uzi huu na wengine wachangie ili tuelemishane vitu vya muhimu vya kuangalia wakati unamtunza mgojwa.

Anatomy binadamu ana sehemu za uwazi, kuanzia macho, masikio, pua, mdomo, sehemu ya haja kubwa na ndogo. Matundu yote haya yanatoa uchafu. Ni lazima yasafishwe kila siku na mengine huhitaji usafi zaidi ya mara moja kwa siku.

Mgonjwa anapokula chakua ni faraja kwako na pia ni dalili za kuwa uhai unaendelea. Kumbuka kuwa hiki chakula na maji ni lazima yatoke nje. Haja kubwa na ndogo huwa zinabeba organic matters ambazo zikiachwa muda mrefu kwenye ngozi huharibu ngozi. Ngozi inalinda mwili, mgonjwa anapopata vidonda huongeza nafasi ya kupata maambukizi ya magonjwa mengine pia kuongeaza maumivu kwa mgojwa.

Mgonjwa asiyeweza kuongea hawezi kusema kuwa amekwenda haja. Unaweza kuweka utaratibu wa kumbadilisha kila baada ya masaa manne. Kumpaka lotion na cream pia husaidia kutunza ngozi.

Unaweza kuwa na vitaulo vya rangi tofauti ili kuepusha maambukizi ya magonjwa. Mfano kitaulo cheupe kwa uso. Blue kwa mwili mzima na chekundu kwa sehemu ya haja kubwa na ndogo.

Unapoanza na maji ya vuguvugu uwe na taulo la kumkaushia, anza kusafisha macho kutoka karibu na pua kitoka nje.Aafishawpaji, pua, masikio na shingo. Mkaushe na umpake lotion. Hapa umemaliza kazi ya kitaulo cheupe. Unakuja taulo la blue. Osha mikono, makwapa, mabega, mgongo, tumbo. Kama ni mwanamke inua maziwa muoshe na kumkausha na mpake lotion.

Unaweza kuhamia miguuni baada ya hapa na baada ya hapo badilisha maji chukua taulo lekundu uanze sehemu za Siri. Mwanaume asiye na tohara vuta ngozi umuoshe vizuri, sehemu ya haja kubwa hakikisha hana uchafu na umkaushe. Paka lotion na mvalishe pad zona chupi ili kumstiri ndiyo umvalishe nguo.
 
Huo ni upendo wa hali juu kwa mgonjwa ...na hata akipumzika kwa amani baraka hubaki nyingi kwa muuguzaji.Asante kwa bandiko mrembo sky eclat
Rafiki yangu mume wake alipata stroke mwaka wa tatu huu ana mhudumia. Aliacha kazi ili aweze kumtunza, bahati nzuri walisha jenga nyumba. Juzi tuliongea kwa kina jinsi kisaikolojia inavyomtesa kuwa mhudumu mkuu wa mume wake.

Kwanza hali ya uchumi imekua mbaya sana nyumbani, pili anapata msongo wa mawazo kuamka, kushinda na kulala na mgonjwa.

Amepata mhudumu aliye mfundisha jinsi ya kumtunza mgonjwa. Amepata ajira kwenye duka la kuuza madawa na wamempa muda wake anaanza sana nne asubuhi mpaka saa kumi jioni.

Anasema ule muda anaokuwa kazini umemsaidia sana kupinguza msongo wa mawazo.
 
Magonjwa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Yanaweza kuwa muendelezo wa magonjwa ya muda mrefu, ajali kama stroke au kugongwa na Gari. Inaweza kutokea kwa mume/mke, Baba/mama au mtoto wako. Si wengi wenye uwezo wa kulipa mtu mwenye taaluma na ujuzi wa kumtunza mgonjwa. Nimeamua kuandika uzi huu na wengine wachangie ili tuelemishane vitu vya muhimu vya kuangalia wakati unamtunza mgojwa.

Anatomy binadamu ana sehemu za uwazi, kuanzia macho, masikio, pua, mdomo, sehemu ya haja kubwa na ndogo. Matundu yote haya yanatoa uchafu. Ni lazima yasafishwe kila siku na mengine huhitaji usafi zaidi ya mara moja kwa siku.

Mgonjwa anapokula chakua ni faraja kwako na pia ni dalili za kuwa uhai unaendelea. Kumbuka kuwa hiki chakula na maji ni lazima yatoke nje. Haja kubwa na ndogo huwa zinabeba organic matters ambazo zikiachwa muda mrefu kwenye ngozi huharibu ngozi. Ngozi inalinda mwili, mgonjwa anapopata vidonda huongeza nafasi ya kupata maambukizi ya magonjwa mengine pia kuongeaza maumivu kwa mgojwa.

Mgonjwa asiyeweza kuongea hawezi kusema kuwa amekwenda haja. Unaweza kuweka utaratibu wa kumbadilisha kila baada ya masaa manne. Kumpaka lotion na cream pia husaidia kutunza ngozi.

Unaweza kuwa na vitaulo vya rangi tofauti ili kuepusha maambukizi ya magonjwa. Mfano kitaulo cheupe kwa uso. Blue kwa mwili mzima na chekundu kwa sehemu ya haja kubwa na ndogo.

Unapoanza na maji ya vuguvugu uwe na taulo la kumkaushia, anza kusafisha macho kutoka karibu na pua kitoka nje.Aafishawpaji, pua, masikio na shingo. Mkaushe na umpake lotion. Hapa umemaliza kazi ya kitaulo cheupe. Unakuja taulo la blue. Osha mikono, makwapa, mabega, mgongo, tumbo. Kama ni mwanamke inua maziwa muoshe na kumkausha na mpake lotion.

Unaweza kuhamia miguuni baada ya hapa na baada ya hapo badilisha maji chukua taulo lekundu uanze sehemu za Siri. Mwanaume asiye na tohara vuta ngozi umuoshe vizuri, sehemu ya haja kubwa hakikisha hana uchafu na umkaushe. Paka lotion na mvalishe pad zona chupi ili kumstiri ndiyo umvalishe nguo.
Elimu nzuri dada Sky Eclat itasaidia wengi.
 
Back
Top Bottom