Kumi bora ya waandishi mahiri wa hadithi za Kiswahili

Emanuel Mashele umesahau, hata profesa Emanuel Mbogo? profesa Mulokozi, Profesa Wamitila ? Hawa watu Muhimu sana kwenye uandishi wa koswahili
 
Kuna mwandishi anaitwa DR. DYABOLI. Huyu jamaa ni moto wa kuotea mbali. Ukisoma kitabu chake kinachoitwa WASOMI WAJINGA utagundua moja kwa moja kwamba huyu jamaa anacheza ligi moja na akina Profesa Kezilahabi na Shaaban Robert. Hao wengine akina Ben Mtobwa na wengineo utawasifia kama wewe sio msomaji mzuri wa vitabu vya nje, hasa simulizi za zamani sana. Wengi wanacopy na ku paste tu kama anavyofanya Shigongo, Patrick CK, Yericko Nyerere na wenzao kibao. Tanazania waandishi wengi wanachofanya ni kutafsiri tu kazi za nje na kuzibadilishia majina na mandhari ili ziende wanavyotaka wao.

Msomeni huyo mwandishi DR. DYABOLI. Hasa hicho kitabu cha WASOMI WAJINGA. Huyu mtu ubongo wake sio wa kawaida.
 
Yaani musiba hayupo top ten yako halafu shigogo yumo?....hujui kitu

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada hujawasoma
Elvis Musiba
John M.S. Simbambwene
Hemedi Kimwanga
Eddie Ganzel
Kajubi Mukajanga
Hammie Rajab
Said Bawji
Hussein Katalambula

Kati ya hawa, Shigongo hamfikii hata mmoja kati ya hawa.
Inaonekana hawajui wote hao

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…