Kumi-kumi za wateule (muziki uliokomaa, muziki ulioenda shule)

Kumi-kumi za wateule (muziki uliokomaa, muziki ulioenda shule)

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mbali na namba yao kuwa na members saba lakini WANNE ndiyo wamesikika zaidi na nitawalezea kinamba, kwa namna ninavyowakubali;

A. KUMI ZA JUMA MOHAMMED MCHOPANGA (MBAKIAJI, X MAN, BISHOO, LYRICIST, FAMOUS, MO JIZZE, SUPER MAN)
1. MVUA NA JUA
2. MAISHA YA BOARDING FT DULLY
3. MSHAMBA FT NATURE
4. TINGISHA FT TID
5. KASIMAMA PEKE YAKE FT SHAKII
6. STORY TATU
7. LONG DISTANCE LOVERS FT DOJO
8. TWENDE KWA MGANGA
9. FAMOUS FT P FUNK
10. MOCUMENTARY
B. KUMI ZA MSAFIRI KONDO (ULAMAA, MWANAZUONI ALOKOMAA, MBUNGE WA MBAGALA, TRAVELLER)
1. SIMU YANGU FT MOE, SOGGY, P FUNK
2. SOLO NA MPENZI FT MR PAUL
3. MTOTO WA DOWNTOWN FT D MONEY
4. KIMA CHA CHINI
5. MDUDU FT BLUE
6. MAMBO YA PWANI FT NATURE
7. MAMBO YA PWANI FT MZUNGU KICHAA
8. UCHU FT DULLY SYKES
9. KILIO CHANGU FT Q CHIEF
10. HUJAFA HUJAUMBIKA FT BANANA, MACK 2B
C. KUMI ZA ALHAJI TAIKUNI ALLY (JAMBAZI M.O.X. MWANGANI TOKA KWENYE KIZA, MCHIZI MOX)
1. SHANGWE FT DOJO NA DOMO
2. MAMBO VIPI FT DOJO NA DOMO
3. SIMBA BADO ANAWINDA - FT J DEAL
4. FALA
5. CHUPA NYINGINE
6. NIKIZIPATA RMX FT WILLY
7. KINYUMENYUME FT DOJO NA DOMO
8. BRAND NEW
9. NATAKA FT K LYIN
10. DEMU WANGU FT NGWEA
D. KUMI ZA JAFARI ALLY MSHAMU (JAFARAI, JAFARHYMES)
1. NIKO BIZE - FT DAZ MWALIMU
2. ANAJUA ANACHOTAKA FT BANANA
3. TOA HELA FT AY
4. UNAWEZA FT NAZIZ
5. SIKU HIZI FT FID Q, ENIKAH
6. UNAPENDA NINI FT FATMAH
7. WAKATI FT CASSIM
8. MY BOO FT Q CHILLA
9. SIYO KWELI FT JIDE
10. TUKO PAMOJA FT UNIQUE SISTERS
E. MARK MALICK (MACK 2B SIMBA)
Amesikika kwenye chorus nyingi za kundi, HUJAFA HUJAUMBIKA ya Solo lakini pia alikuwa akifanya audio production pale Sound Crafters. Wakati wezake wakirap, yeye alikuwa mlevi wa Ragga.
F. KELVIN KIMARI ( K MARIS, KEVI)

Amesikika kwenye ngoma za kundi lakini kwa uzuri kabisa msikilize kwenye WATU KIBAO. Sina ngoma hata moja aliyofanya peke yake.

G. LADY LOU
Kama Mack 2b, huyu pia alikuwa mlevi wa Ragga. Hakufanya kazi nyingi Sana na kundi na angalau ngoma zake binafsi zilienda kwenye media na kumtangaza kama solo artist.

NGOMA KUMI ZA KUNDI
1. TUMERUDI TENA
2. WATU KIBAO
3. USIPIME
3. NANI KACHAFUA HEWA FT SHAKII
4. HIP HOP NA RAGGA
5. BAMBIKA FT SHAKII
6. MSELA
7. VILE VILE
8. WABAKIAJI
9. MANGIRIMA WITH KALAMASHAKA
10. HII GAME WITH K'SHAKA, XPLASTAZ

STORI KUMI ZA WATEULE
1. Moe aliwahi kusema key figures wa kundi ( MOE, MOX, JAFA na SOLO) wote ni left- handed "mashoto"
2. MOX na Majani ni mada kubwa. Nawaza mpaka leo, Majani aliona Jafa ni mkali kuliko Mox?? Nawaza MOX aliwezaje kwenda KUIFANYA ngoma iliyokuwa yake iliyoboreshwa na Ngwea palepale kwa Majani aliyemtosa miaka yote halafu baada ya ngoma kuitika mtaani, Mox akaifanya yake na kuamsha moto!! Nazungumzia MIKASI.

MOX aliyezinguliwa na Majani, alirekodi ngoma nyingi kwa Shakii na baada ya hapo akafanya ngoma kadhaa kwa MAN TSUKI - TBT RECORDS, MJ na kwa Lamar. Kubwa kuliko yote, BILA MAJANI, BADO TUNAMHESHIMU MOX MPAKA LEO ( kwa sauti yake mwenyewe; MUNGU S'O KHALFANI AKA MAJANI)

3. Moe na wizi wa nyimbo; anzia pale kwenye KAMA UNATAKA DEMU VS MABINTI DAMUDAMU ya MWANAFALSAFA, njoo kwenye CHEZA KWA STEP vs ngoma ya MICHAEL JACKSON aliyoibeba tone mpaka bridge, DON'T STOP TILL YOU GET ENOUGH, toka hapo njoo kwenye LONG DISTANCE LOVERS VS PART TIME LOVER ya STEVIE WONDERS halafu malizia na MSELA VS OYA MSELA ya THE MAWINGU BAND. AU KULIKUWA NA MAKUBALIANO HIVYO HAKUIBA, AU NI SAMPLE TU??

4. Solo na Moe na mkali wa rhymes 2004; lile shindano la Shigongo liliibua SINTOFAHAMU kubwa. Wengi hawakukubaliana na matokeo lakini Solo alizidi. Kampaka Sele kwenye ngoma nyingi kuliko wasanii wote. Kwa mtazamo wako, UNGEMPA nani ubingwa ule?

5. JAFARAI ana ngoma ngapi alizofanya mwenyewe? Yeye na TEMBA nani anaongoza kwa kushirikisha wasanii wengine kwenye ngoma?

6. NAZIZ alikuwa member halali wa kundi? Au alikuwa anapewa shavu tu? Katokea kwenye ngoma nyingi za WATEULE. Ana undugu wa damu na Jafa au ulikuwa ukaribu tu wa kikazi?

7. Waliitwa WATEULE baada ya kushinda kwenye mashindano ya Rap na kutakiwa KUTENGENEZA kundi. Ningekuwa na nafasi ya kuwachagulia jina basi ningewaita SAUTI KAVU au RAW VOCALS kutokana na sauti zao za awali japo Moe na Jaffa walibadilika, MOX na Solo wamebaki na sauti zao zilizowatambulisha kwenye game.

8. Kulikuwa na nyepesi-nyepesi mtaani kuwa SOLO,MOX na MOE walimponda JAFFA kwenye BADO YUKO VILEVILE na yeye akawajibu kisela kwenye vesi ya mwisho ya MCHARUKO FT WYRE, Je ni kweli?

9. WATEULE ni kundi ambalo linatofautiana na mengine kwenye solo projects. Wakati wengine wamekuwa wakipeana MASHAVU kwenye ngoma binafsi, hawa WASHKAJI wao walifanya Kolabo zaidi na watu wa nje ya kundi. MOX kafanya zaidi na Dojo na Domo. Moe alikuwa na ukaribu zaidi na Ngwea na kuwa kama na kundi dogo la watu wawili, Jafa kafanya ngoma nyingi na the first lady, NAZIZ wakati Solo alikuwa anachanganya wasanii TOFAUTI.

10. WATEULE NI MIONGONI MWA MAKUNDI MACHACHE AMBAYO YANA SKENDO SIFURI.
WASANII WAMEPITA KWENYE MADIMBWI TOFAUTI KAMA; KULELEWA NA MISHANGAZI, KUFANYA VITUKO STEJINI NA SASA WIMBI LA USHOGA BUT THE BROTHERS COME OUT CLEAN KWENYE MASOO YOTE HAYA.
SIFA YA PILI YA WATEULE NI MITUPIO. WAZEE WANAJUA KUZINYUKA HAWA; SI MOX, SI JAFA, SI SOLO WALA MOE, TENA HUYO NDO KABISAAAA!

NI MUDA MREFU JAFA ALITANGAZA KUWA NA CAR WASH, MOE AKAJA AKATUAMBIA KUWA NI BABA MWENYE NYUMBA WA IRENE UWOYA, MOX NI MJASIRIAMALI NA ANAJITANGAZA SANA MTANDAONI WAKATI SOLO YUPO ZAKE KIWANJA.

MACK 2B NA LADY LOU WALITANGULIA MBELE ZA HAKI NA BROTHER KEVI SINA TAARIFA ZAKE.
Bonus; Jafa alikuwa na MCHUMBA wake aliyeitwa Shy Rose Bhanji, basi zile vidoes Kali za Jafa na pamba, Wana WAKASEMA Shy ndo alikuwa anasimamia show. Sijajua ukweli wa hili. Miaka ikaenda, shy akaingia bungeni, Mara Sugu akapita na Shy.

Jafa alilalamika mpaka redioni. Nay wa MITEGO akawapitia wote watatu kwenye ngoma yake.
Aseee! Nilitaka kusahau!! Nina mwanangu nimekutana naye sekondari miaka hiyo, anaitwa AFISA MWAIPOLE (AFIZZY MTENGWA) basi huku na kule zikaanza stori za game ya kitambo.

Mwana akamtaja MOE Kama RAPA WAKE NAMBA MOJA BONGO. Nilishtuka sana maana sikuwahi kuona MOE ana MASHABIKI binafsi tena wa kumwona kama namba moja. Nikamchana kuwa MOE HAKUWA NA LOLOTE ILA ALIKUWA MKALI SANA KWENYE NGOMA ZA KUSHIRIKISHWA.

Kumbe mwana alikuwa na albums za Moe Kama zote magetoni. Akaangusha orodha hapo mpaka nikaanza kumwita JAY MOE na urafiki wetu ukakua kuanzia hapo.

Alidata sana nilipomwambia RAPA NILIYEKUWA NIKIAMINIA NJIA ZAKE ALIKUWA GEEZ MABOVU basi kuanzia hapo akawa ananiita MABOVU mpaka leo.

ASEE MIMI NI MTEULE, MIMI NI MBAKIAJI, MUZIKI WANGU UMEKOMAA NA UMEENDA SHULE.
LUAH SANAA
MWANDISHI WA AINA YAKE.
130523.
1684302359926.jpeg
1684302372070.jpeg
1684302528698.jpeg

1684302541765.jpeg
 
Big up kwa Andiko zuri,..kwangu Wateule ni moja ya makundi bora ya muda wote kwenye muziki wa Bongo...

Malegend hawa...
 
Back
Top Bottom