Edward Marekani
New Member
- May 30, 2021
- 2
- 3
Nazungumzia kumilikiKuna muuzaji na mmiliki wewe unauulizia yupi?
Si lazima uwe umesomea pharmacy ili kumiliki pharmacy. Ila ili kuweza kuuza inabidi umuajiri mtaalamu wa Pharmacy aliyesajiliwa na bodi ya wafamasia Tz.Nazungumzia kumiliki
Yoyote anaweza akamiliki ukilipia leseni na mapato kwa halmashauri ila kuuza lazima usomeeNazungumzia kumiliki
DahKumiliki duka sio lazima uwe umesoma pharmacy, ila unatakiwa kuwa umesomea umiliki. lakini kuuza dawa zake lazima usomee mafunzo ya ADDO, sijui kwa siku hizi wanaitaje. ila kumiliki pharmacy lazima mfamasia ahusike, kama sio wewe basi ingia naye makubaliano awe kama partner uwe unamlipa kila mwezi kifutajasho (ambacho kwa sasa sio chini ya Tzs 1,000,000/= naongea kwa uzoefu kwasababu ninayo maduka ya dawa)
La sivyo hutaruhusiwa kuuza baadhi ya dawa kwenye duka lako la kawaida (DUKA LA DAWA MUHIMU). kupata nafasi ya kuuzia, ni mbinde, mafamasia lazima wakulambe pesa sana, hata ukaguzi wa chumba chake kuna masharti yake watatembelea na kuangalia na kuna umbali unahitajika toka duka moja kwenda lingine. hao jamaa ni miungu watu balaa, hadi nakuonea huruma.
Sio lazima uwe umesoma pharmacy, lakini kuna short course ya kama wiki hivi,ambayo ukimaliza utapatiwa cheti cha umiliki wa duka la dawa muhimu.Hii course hutolewa kwa yeyote yule aliyefikisha umri wa miaka kumi na nane.
Kuna njia nyingine zisizo halali sana,kama kutumia vyeti vya wengine kusajilia na kumiliki duka la dawa muhimu,lakini nadhani zinacomplications zake.
Asante kwa Tangazo.Inasikitisha sana fani hii ya pharmacology inaingiliwa na kila mtu.
Tatizo ni kuwa wafamasia hawajajitokeza kuelezea na kutetea umuhimu wao ktk kuhakikisha wanatambulika kama wataalamu wa fani hii ya madawa.
Hata website ya serikali inayoelezea nafasi ya wafamasia katika kushiriki katika kuwapatia watanzania huduma bora na salama hakuna taarifa za kutosha.
Wafamasia wanashindwa kueleweka umuhimu wao ktk jamii ya kiTanzania tofauti na fani zingine zinazoheshimika na kufahamika kama za manesi na madaktari wa binadamu . Hata ka website cha school of pharmacy MUHAS Publications kana sikitisha.
Wafamasia Tamzania wanaonekana hawana tofauti na wauza mizizi na magome ya dawa za kienyeji .
Angalau Dr. Idris Mtulia alijitahidi na kuacha legacy ktk fani ya pharmacology:
Pharmacology & therapeutics: A manual for medical assistants and ...
Pharmacology & therapeutics: A manual for medical assistants and other rural health workers (Rural health series) [Mtulia, I. A. T]
Hakuna Fani Inaitwa Pharmacology , Ni Pharmaceuticals ScienceInasikitisha sana fani hii ya pharmacology inaingiliwa na kila mtu.