Kumkopesha mwanamke inahitaji akili

DON SINYORI

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2016
Posts
511
Reaction score
417
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp...!

_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._

--
_*Kisha nikaituma ile message*_

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake... Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

*Akatuma message akiniuliza...*

_Hao wanawake unawajuwa, ...mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli...!_

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa...!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa...! Akaniandikia message nyingine....

*...Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe... Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri...!*

Nami nikamjibu...

_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo...!_

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai...!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa.... Kama sio mie!
 
Hapo ulimpatia,maana ukiwadai sana wanaanza kusambaza habari kwamba unamtaka ila yeye hakutaki.Usithubutu kumkopesha mwanamke/msichana, labda kama umeamua kutoa sadaka,maana hata akiweka dhamana kitu bado anaweza kukugeuzia kibao na jamii haitokuelewa hata kidogo.
 
Tupe na mbinu ya kulitoa taifa lenye utajiri wa madini na rasilimali kwenye umasikini, umetisha mkuuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
sasa unamkopesha kwan taasisi za mikopo hamzioni mbona unafanya biashara na unakwepa kodi na unajitangaza
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] kweli ulimpatia sana
 
Hiki kichekesho kimeshazunguka sana whatsApp
 
Kwa nini wanawake wanakuwa hivyo? Nilikuwa sijui ila juzi juzi nimeelewa hadi namuonea huruma mdada wa watu anavyohangaika na deni. Nimefunga rasmi zoezi la kukopesha mwanamke nikiwa na fursa kidogo nitamsaidia tu. Kukopesha mwiko, Maana majaribio yangu kama matatu ya kukopesha yameishia madeni ya kudumu kama la taifa (samahani sichochei mtu)
 
absolute fact mkuu
 
Daaaaah
Nmecheka xn
Mm nilitaka nmkopee demu kama twenty hv ila nkasita kumbe baada ya cku moja demu kahamia kjjn
Aisee nashukuru mungu cku mpa
 
Vpi nae kaolewa kwan mkuu
Alisha lipa mkuu hii njia ni nzuri itumieni mimi alinilipa siku hiyo hiyo saa 20:09 ndo niliona M-Pesa sms ila hajolewa ana mshkaji wake waga anakula mzigo.
 
Asante mkuu....cku yangu imepita vzr[emoji28]
 
Hii ndio ubunifu unaotakiwa. Vinginevyo pesa yako ungeisikia hewani jombaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…