Kumkumbusha mke maagizo kwa kutumia maandishi kwenye karatasi

Kumkumbusha mke maagizo kwa kutumia maandishi kwenye karatasi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Kama mnavojua binadamu tumetofautiana uwezo wa utambuzi na uwezo wa akili.ndo maana wengine wanasahau sahau unakuta amekaa sehemu kainuka kaacha simu anafika mbele anashtuka kama kasahau simu anarudi kuitafuta..Ila kuna hao wengine ikiwemo mimi labda tu niwe nimelewa ila nikiwa sijanywa niko makini sana huwa sisahau sahau mipango yangu daima natembea nayo kichwani..


Assume sasa umeshaoa umempenda mke ambaye anasahau sahau maagizo unayompa ya kuendesha mambo ya home inabidi ule udhaifu wake uubebe. Jamaa yangu tulikuwa tunapiga naye stori akadai mkewe akimwambia labda fanya kitu fulani akirudi anakuta mke kasahau.mambo mengi kanitolea mfano kuna usafi labda wa kitu fulani au kununua kitu fulani. Yaani majukumu ya kawaida yale ya nyumbani anasahau sii kwamba anafanya kusudi ila tu msahaulifu.

Sasa ndo swali kwenu wana jf je mke wa hivyo ni sahihi kuwa unamsisitizia maaagizo kwa njia ya ki note, yaani kabla hujaondoka unaandika maagizo unayaacha mezani.

Kwamba mama watoto
1. Upeleke mtoto akapime uzito

2. Utafute mzoa taka aje azoe nisizikute.

3. Ununue na mtego wa panya

4. Ulipie na bill ta maziwa

5. Uzime pump ya maji ikifika saa 4

6. Bye mke wangu nakupenda usisahau

Ataona umemdharau ikiwa nia yako tu umzoeshe kuwa anakumbuka.
 
Back
Top Bottom