marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,019
- 1,824
KUMPA MARIANO DIAZ JEZY NAMBA SABA(7) MADRID NI DHARAU.
DHARAU ni kitu kibaya sana. Mashabiki wa Real Madrid wamemkasirikia rais wao, Florentino Perez wakimwambia amewadharau sana.
Unajua kwanini? Kisa ni mchezaji Mariano Diaz.
Ishu si kumsajili Mariano, bali kwa kitendo cha rais huyo kuamua kumpa mshambuliaji huyo jezi yenye heshima kubwa klabu hayo, jezi yenye Namba 7 mgongoni.
Staa aliyekuwa akivaa namba hiyo hapo kabla ni Cristiano Ronaldo na aliwahi kuivaa pia Raul, lakini kitendo cha kumpa Mariano jezi hiyo kimetafsiriwa na mashabiki wa Los Blancos ni dharau iliyopitiliza.
Ronaldo kwa sasa ametimkia Juventus, ambako pia amekwenda kukabidhiwa jezi namba 7. Kwa kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi cha Real Madrid, Ronaldo amefunga mabao 450 katika mechi 438 alizocheza kwenye timu hiyo na kubeba mataji 14 makubwa.
Mara ya kwanza alitua Bernabeu mwaka 2009, Ronaldo alikabidhiwa jezi Namba 9, kwa sababu kwa wakati huo Namba 7 ilikuwa ikivaliwa na Raul.
Kuna baadhi ya timu zimeamua kuzistaafisha jezi zilizovaliwa na magwiji wao kwa kuonyesha heshima kubwa, lakini Real Madrid ambayo ipo chini ya Kocha Julen Lopetegui imeamua kumpatia jezi ya heshima mchezaji wake mpya ambaye hana uzoefu wowote.
Mashabiki wa timu hiyo walionyesha hasira zao kwenye mitandao ya kijamii baada ya Real Madrid kutuma video ya utambulisho ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akiwa na jezi yenye Namba 7 mgongoni.
Mashabiki kibao walitumia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii kuishambulia Real Madrid kwa uamuzi huo wa kumpa mchezaji mwenye uwezo wa kawaida jezi iliyovaliwa na magwiji wa timu hiyo.
Shabiki mmoja aliandika: “Hizi ni dharau kubwa kwa klabu na kwa gwiji wa kipekee, Cristiano. Ni aibu kubwa kwa klabu na historia yake.” Mwingine aliongeza: “Ukosefu wa heshima mwingine kutoka kwa Florentino Perez kumpa jezi Namba 7 mchezaji Mariano.”
Lakini kuna shabiki mmoja alijipa matumaini baada ya kusema: “Pengine itamfanya acheze kama Ronaldo...labda.”
Ronaldo ameifanya jezi Namba 7 kupata umaarufu mkubwa na kuamua kuitumia kama nembo kwenye biashara zake akianzisha kampuni inayokwenda kwa jina la CR7.
Baada ya kutua Juventus, mchezaji Juan Cuadrado, aliyekuwa akivaa jezi hiyo yenye Namba 7 mgongoni alikubali kubadili na kumpa Ronaldo kutokana na heshima ya supastaa huyo wa Ureno. Ronaldo ametua Juventus kwa ada ya Pauni 88 milioni.
Mashabiki wa soka duniani wanachokiona ni kama kutakuwa na mtu mwenye presha kubwa kwa sasa basi ni Mariano, ambaye amerudi Madrid kwa Pauni 23 milioni akitokea Lyon na kukabidhiwa jezi hiyo nzito.
Akiwa Lyon, Mariano alifunga mabao 21 katika mechi 45 alizocheza kwa msimu uliopita na kiwango hicho ndicho kilichoishawishi Real Madrid kumsajili tena baada ya kukosa huduma za mastaa kadhaa walioripotiwa wangenaswa kuchukua mikoba ya Ronaldo ambao ni Eden Hazard, Kylian Mbappe na Neymar.
[Source www.instagram.com/mwanaspotiapp]