Kumpoteza mtu unayempenda!!

Whatever problem/difficult i face in my life including those related to relationshis,i always remember that:

God uses problems to PROTECT you.

A problem can be a blessing in disguise if it prevents you from being harmed by something more serious. "You intended to harm me, but God intended it for the good. Genesis 50:20.

God uses problems to PERFECT you.

Problems, when responded to correctly, are character builders. God is far more interested in your character than your comfort. Your relationship to God and your character are the only two things you're going to take with you into eternity. "We can rejoice when we run into problems ....they help us learn to be patient. And patience develops strength of character in us and helps us trust God more each time we use it until finally our hope and faith are strong and steady." Romans 5:3-4

Here's the point:
God is at work in your life - even when you do not recognize it or understand it. But it's much easier and profitable when you cooperate with HIM.
 

Jamani nnunu, shukrani sana mpendwa..maneno yako ya faraja na nimelia wewe mpaka muda mwingine nikitaka kulala usiku machozi yanatiririka..kweli ni changamoto, naomba Mungu nimsamehe na kutoendeleza hasira..



kama vile unausemea moyo wangu kipindi hivi.

Imewahi kukutokea mpendwa?kweli mapenzi kizungumkuti



mpenzi nashukuru sana..nimeshindwa mwenyewe kuelewa kama ni upendo au hakuvutiwa na kitu ila suala linabaki pale pale angeniambia ukweli hakika nisingeweza kumng'ang'ania..Okay alinitafuta baada ya kuoa na kutaka kunipa maelezo, jamani kweli hiyo ina maana gani?!au ndiyo kutaka kujisafisha wakati ni too late..
kusahau na kusamehe inasaidia sana vinginevyo sijui tungeishije..mapenzi kweli ni milima na mabonde, tunapitia mengi! Mola aniongoze! ubarikiwe mpz
 

Pearl dear, thanx in deed nimepitia hiyo nakala..Thanx for sharing as well ktk kipindi hiki!


all i can tel u jus move on wid lyfe,everythg has reason in this world that is why God has decided 2 b that way.ma dea stop stressing urself make urself happy jus 4get abt him nd move on its nt the end of world!

Salma mamii, thanks. Sure, I have to move on mana that's the reality!!.I'm so glad distance inasaidia mana vinginevyo sijui ingekuwaje kuwa nae hata mji mmoja..


Naumia kama vile ni mimi. Pole BJ. Fanya maombi sana, yatasaidia kuondoa hizo hasira. I hate wanaume matapeli wa mapenzi!!! Ni vile hatuwezi kuwatambua, wanajua kuigiza hao. Laana yetu na iwe juu yao.

Sweety hapo mimi ndiyo nilipoumia, kwanini hakuniambia hata kama kuongea angeshindwa hata email angeniandikia au kumtuma mtu..kweli hata yeye nikimweka kwenye nafasi yangu sasahivi sijui angekuwaje?!!!...He was so nice, charming and loving to me!..ila vyote amefunika na ukatili aliofanya!Huyu mwanaume,mmh nakosa jibu kabisa..
Nafanya maombi, Mungu kwa kila kitu maishani mpaka leo na aniwezeshe kukabiliana na hii hali..thanx mamii!!
 

BAK, thanx a lot..kweli nilimpenda sana, kumjali na kumshirikisha kwenye mambo mengi kama alivyofanya...tena mbele ya macho na masikio yangu tulikubaliana mwisho wa 2011 tufanye kweli kuwa wanandoa. yani hiyo nimeenda kumsuprise ilikuwa ndiyo atanivisha pete mana tulitaka tufanye 'gathering' kidogo kwa vile tulipanga kumbe nikakutana na kisanga kingine..

Tangia nimemjua sijawahi kujutia kuwa nae mpaka baada ya hiki kitendo, yani tumekuwa na muda mwingi wote na muda mwingine mwingi tulikuwa mbalimbali ila sikuwahi kuona kitu cha ajabu kama nimemkwaza mpaka akanitamkia neno la kuachana au la..japokuwa nina mapungufu yangu kama binadamu wengine lakini siyo kutelekezwa hivi..so painful!!

For sure 'they say love hurts, but it is still the people behind that so called love who really hurt you'

Thanks for the clip as well, brilliant message!!
 
pole sana mpenzi
lakini ni safari wengi hupitia ni wachache sana wenye
bahati ya kupata mweza tangu mwazo naelewa machungu
unayopitia, vitu kama hivi vinaweza hata vikufanya uwachukie
wanaume wote, au unaweza hata kusema mi siolewi kabisa..

my dear
hatuna uwezo wa kusoma akili za watu
kwani tungekuwa na huo uwezo tungeepuka mengi..
na penzi ni kitu ambacho hatuwezi kukikimbia kabisa
kama we hutaa kaa upende atajitokeza akupendaye..
inauma sana pale penzi linapoenda upande mmoja ..

Sweet
Itakuchukua muda sana na inaweza kukuletea matatizo
mengine mengi, huu ndio wakati wa we kukaachini na
kujiangalia ni nini BJ anataka maishani, mpenzi anza ku
consecrated on you.. my dear your happiness comes first.
 
Pole sana Belinda! Kitu pekee tunachowezza kufanya ni kukupa moyo na kukufariji. Umefanya vizuri kulileta swala hili hapa kwani moja katika mbinu za kuponya ni kulizungumza hili na marafiki na jamaa zako. Kwa upande wangu, ninaungana na wale waliosema kwa namna moja au nyengine "Hata jambo baya lina uzuri wake", nikimaanisha kuwa "hukuwa unastahiki kuishi na mtu asiyejali kama huyo". Ni vyema kuwa hili limetokea mapema; Mungu kakuepusha na majanga mengi. Fikiria angekuja kukusaliti baada ya kufunga naye ndoa!, maumivu yake yangekuwa makali zaidi.

Baada ya kuondokewa, utapitia katika hatua hizi nne:
1. Kutoamini na kutokubali kilichotokea lakini ndio ukweli.
2. Kwa kuwa ndio ukweli, hili litakuuma sana,
3. Maumivu yataambatana na huzuni.
4. Mwisho utakubali matokeo na ukweli wa mambo. Ni maji yaliyomwagika.

Kwa ushauri jinsi ya "kukusanya vipande vya moyo uliovunjika", fanya baadhi katika haya:
- Kila unapowaza kuwa "Ninampenda na siwezi kuishi bila yeye", utakuwa unakumbuka mazuri tu uliyoyapata na mliyogawana kabla ya mambo kuharibika. Lakini kama unavyokiri kuwa "mlikuwa na matatizo yenu madogomadogo", ukweli ni kuwa hayakuwa madogo kama ulivyokuwa unafikiria. Yalikuwa makubwa lakini ukavumilia kwa sababu ulikuwa unapenda. Sasa ni wakati wa kuyafikiria haya kwa lengo la kukutoa katika mawazo ya kuwa kulikuwa na mazuri tu. Hii itakusaidia umuone kwa jicho jengine.

- Kimbilio lako la mwanzo iwe paketi za tisues - lia kadiri uwezavyo. Jifungie chumbani kwa muda unaotaka, hata masaa 24 mfululizo, lakini ukitoka hapo, jufute machozi na kumbuka "Maisha yanaendelea". Kama ulivyokwisha shauriwa kabla, kimbilio lako la pili iwe marafiki, wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Hakuna tiba nzuri kama kupata bega la kulilia, hasa likiwa la mama, dada, au rafiki. Pamoja nao au peke yako, tembea/tembeeni sehemu za wazi. Epuka vilabu kwa kipindi hiki.

- Kama una uwezo, tafuta mnyama wa nyumbani, hasa mbwa au paka. Huyu atakupa mapenzi yote bila kukudai saaaana zaidi ya mlo wake na kumjali.

- Jiunge na kozi, masomo au amali ambayo daima ulikuwa unahamu uifanye. Muda wako mwingi utakuwa unashughulika na hili badala ya kukaa kumfikiria au kusubiri miujiza...AMESHAOA,hakufai, hakustahiki.

- Fanya kazi za kujitolea kama vile kuwahudumia wazee, watoto na makundi hitaji.



KANUNI YA DHAHABU: KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUUGUZA, USIMSOGELEE; USIMTAFUTE; USIMRUHUSU KUTAFUTA FARAHA NA WEWE NA KUMWACHA AKUMWAGIE UONGO
 
Jamani hii dunia ina vituko,

Ni jambo la ajabu binadamu kumfanyia mwenzio mambo ambayo kwa hakika wewe mwenyewe si tu usingeyapenda bali usingemudu kuyakabili.

Hata hivyo sitashangaa baada ya muda si mrefu kumsikia narudi na nyimbo za kshenzi shenzi kuomba msamaha.....Nin ushahidi wa watu wengi wa namna hii (wakiwemo ME na KE) ambao wameishia kuishi maisha yao yote na vivuli vya wachumba wao waliowatenda.

Cha msingi BJ ujiandae kumweleza kuwa hakuwa wa kwako na nafasi yake ameizamisha baharini mwenyewe. Kama unaweza, basi msikilize ili upunguze maswali kibao kichwani...ILA SIKU ZOTE MWELEZE KUWA...HE CAN GO TO HELL AND NOT BACK TO YOU.

Mzee DC.
 
Pole sana ndg yangu, jipe moyo mkuu, mume wako atakaye kupenda na utakayempenda zaidi ya huyo Mungu anamjua ndiyo maana hakuruhusu uolewe na huyo, wewe ulidhani ndiye kumbe huyo si mume wako. Muombe Mungu usamehe yote na uachilie kabisa then utamshangaa Mungu, pole ila jua yupo utakayempenda kuliko huyo, ataletwa kwako mara. Vumilia kidogo
 

Ndugu yangu asante kwa maono yako. Naomba nikwambie kitu kuwa mimi ni mtu mzima, ingekuwa tumekwaruzana na kuachana wala nisingejisikia hivi. Mimi siyo malaika ila sioni kitu gani nimechangia cha ajabu mpaka kushtukizwa hili jambo. Pia kumbuka angeniambia mbona ningeumia na kujiandaa kiakili hatimae kukubaliana na hilo suala mana nisingeweza kumzuia hata kama nampendaje.

Nimejaribu kutoa short story mana nimeshindwa kuielezea kiundani zaidi kwa vile imetokea karibuni. Nilivyoiweka hii issue ni kuwa nimeshtushwa na jambo la mwenzangu kuoa wakati tulikuwa serious sisi kuoana mwishoni mwa 2011, sijui imenipata. Sasa kama alikuwa na tatizo najiuliza kwa nini hakunishirikisha? kama vile kuniambia tisingeweza kuwa wote au kampenda mtu mwingine na hivyo mimi na yeye basi. simpo as that!

Kweli tulikuwa serious na sijawahi kupinga jambo lolote kuhusu ndoa alivyogusia na tukakubaliana..unajua nini, natamani mwenyewe nipate jibu la hili swali ila sina kwa sababu ukweli anaujua mwenyewe jamaa. Hata kama angeniumiza kuambiwa ukweli ila ungesaidia sana na ningekabiliana nao na maumivu yake.

Shukrani kwa mtazamo wako..
 
Reactions: Mbu
I can feel u...i am going through the same thing....:'(
 

Red: Sio rahisi kama unavyodhani kwa mtu kumface mtu kumweleza ukweli kwamba anataka akuache na ana mchumba mwingine, ukizingatia alishakuahidi. Alichokifanya jamaa ni kama wengi wafanyavyo. Msamehe bure tu.

Blue: Ni kwakuwa hukutaka kumsikiliza alipotaka kukueleza what happened, then itaendelea kukutesa rohoni hadi uujue ukweli. (Kama utataka kumpa nafasi ya kukueleza kilichotokea, which is good to know. itakusaidia kupunguza donge ulilonalo).
 
Mapenzi yanaumiza sana nashindwa kujua kwa nin mtu anaahid kitu ambacho hawez anajua hawez timiza anakupa tumain baadae anakugeuka anakuumiza! Pole sana mpendwa yametukuta hayo umenikumbusha mbali sana, usikate tamaa utampata ambaye atakusahaulisha yote chaguo toka kwa mungu shukuru tu kwan ujue kuna jambo mungu kakuepusha simama kuwa imara futa machoz endelea mbele!
 

Mi nashauri asimtafute, itamuumiza zaidi, vip akiambiwa kuwa sikuwahi kukupenda au

mchumba wangu alikuwa mbali ndo maana nikawa na wewe acha kabisa ataumia sana, hata kushinda JF inapunguza stress,
 
Ukisha maliza kulia, ukatulia, unatakiwa umshukuru Mungu sana kwa kukuepusha na mume wa aina hiyo. Mtu msiri wa kiwango hicho ni mbaya sana kuwa mumeo. Imagine amekuwa na wewe kipindi chote hicho (sijui mmekuwa pamoja kwa muda gain), bila hata kukuonyesha dalili kwamba anakulamba kisogo. Ukamwamini kwa 100%, kumbe hata mpango wa kukuoa hana!.. Hao ndio wanakuwaga na mahusiano nje ya kudumu bila wife kuhisi. Manake kwa wife anawajibika ipasavyo na kule kwingine ana mwanamke na watoto kibao. Unakuja kushangaa tu siku ya siku mumeo kumbe ana watoto 3 nje tena wa kwanza ana umri kama first born wako! Aina ya Shenzi ….
 
My dear BJ kila jaribu lina mlango wake wa kutokea, omba uonyeshwe mlango!
 
pole ma dia lakn you need 2 go on wit ur life whether u like it or not!! wote 2lipitia huko na 2liumia sana lakini sasa 2meshayaweka pembeni na 2nasonga mbele kabsa. hata ukiendelea kukaa hivyo imeshatokea na haiwezi rekebishika!!!! continue wit ur life ma dia, that is ma advice 2u!!
 
dah! sijui kwanini nimeishiwa na maneno baada ya kuona hii sred na kugundua kwamba alieleta hii sred ni mrembo BJ.
all I can say for now. pole sana BJ and be strong to face it.

dah! hakyanani wazembe wengine ni wa kulogwa tu.
 
Reactions: Mbu

...wengine akili zinapowarudia, hujishtukia wameshaoa. Kwani huyo jamaa alioa kisiri siri kiasi kwamba
hata mashoga zako hawakujua/kukwambia? ...move on with your life. Why are you allowing yourself to be stuck in the past?

...kujiuliza kwanini ilhali majibu huna ni sawa na kung'ang'ania kupanda ndege iliyokwisha ruka.
tupa hiyo boarding pass, mlaani shetani usubirie usafiri mwingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…