JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kanuni ya adhabu inaeleza kuwa iwapo kosa limetendwa, kila mmoja wa watu wafuatao atahesabiwa kwamba ameshiriki katika kutenda kosa hilo na atakuwa na hatia juu ya kosa hilo na anaweza kushtakiwa kwamba amelitenda.
Watu hao ni pamoja na:-
(a) Ambaye ametenda au ambaye ameacha kutenda kitendo ambacho kimepelekea kosa hilo;
(b) Mtu yeyote ambaye ametenda au ambaye ameacha kutenda kitendo chochote kwa ajili ya kumuwezesha au kumsaidia mtu mwingine kufanya kosa hilo.
(c) Mtu ambaye amesaidia mtu mwingine katika kufanya kosa hilo;
(d) Mtu yeyote ambaye ameshauri au kumfanya mtu mwingine yeyote atende kosa hilo, mtu huyo anaweza kushtakiwa kwa kufanya kosa hilo au kwa kushauri kosa hilo litendwe.
Upvote
1