Kumshawishi Mfadhili kwa Kubadili Mtazamo Wake

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60


Mtazamo ni picha/tafsiri tunazojenga katika fikra zetu kuhusiana na watu, vitu, mawazo, vitendo n.k. Mtazamo ni kipengele muhimu sana katika mchakato wa kutafuta ufadhili, na kila mhusika katika utafutaji wa ufadhili ndani ya Taasisi anapaswa kuwa na ufahamu juu ya hili.
Katika ufadhili (fundraising), kuna nadharia zifuatazo ambazo zinaeleza kuhusu kubadili mtazamo katika ufadhili, nadharia hizo ni;
  • Expectancy-Value Model: Nadharia hii inasema kwamba, mtazamo wa mfadhili wa kuchangia Taasisi au kutokuchangia huweza kujengwa kwa kuhakikisha kwamba; kunakuwa na uhusiano wa moja kwa moja kati ya ufadhili unaoombwa na matokeo yatakayotokea. Kwa mfano; unahitaji ufadhili wa vyandarua ili kukomesha ugonjwa wa Malaria, Je ufadhili wa vyandarua utaenda kutokomeza Malaria? Ni suala la kujiuliza ikiwa unataka kubadili mtazamo wa Mfadhili.
  • Appraisal - Based Model: Nadharia hii inasema kwamba mtazamo wa mfadhili wa kuchangia Taasisi au kutokuchangia unategemea manufaa au matokeo atakayopata, kwa mfano; uanachama, zawadi ndogo ndogo kama kofia, t-shirt, kadi, kutambua mchango wake, mrejesho/uwazi juu ya matumizi ya fedha n.k
  • Means - End Chain Theory: Nadharia hii inasema kwamba; uamuzi wa mfadhili kuchangia au kutokuchangia Taasisi unategemea uwiano wa dhumuni la mradi (Project Purpose) na "interest" ya mfadhili. Kwa mfano unahitaji ufadhili wa miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira, ni ngumu kubadili mtazamo wa Mfadhili ambae "interest" yake iko kwenye masuala ya sanaa.
Lengo la "fundraising Appeal" ni kubadili mtazamo wa mfadhili, kutoka kutokufikiria kuifadhili Taasisi na kumfanya aone kwamba anawajibu na analazimika kufadhili . Kuna mbinu nyingi hutumika kubadili mtazamo wa Mfadhili, miongoni mwazo ni;
  1. Mawasiliano (Communication): Kubadili mtazamo wa mfadhili huweza kufanyika kwa; kuhakikisha maombi ya ufadhili "Fundraising Appeal" yanafanywa na mtu mwenye nafasi kubwa ndani ya Taasisi au kuweka msisitizo mkubwa juu ya ubora, uzoefu na ufanisi wa Taasisi.
  2. Ujumbe (Message): Hapa kuna aina mbili za ujumbe, aina ya kwanza ni "one side of argument" ambayo ujumbe hueleza upande moja tu ambao ni matokeo ya ufadhili (Positive Impacts). Aina ya pili ni " two-sided argument" ambayo ujumbe hueleza pande mbili kwa maana; matokeo yatakayotokea baada ya ufadhili na hasara zitakazotokea endapo ufadhili utakosekana. Kila aina ya ujumbe hutegemea na hadhira (mfadhili). Tafiti zinaonyesha kwamba "one-side argument" ni nzuri kwenye kubadili mtazamo wa mfadhili mwenye elimu ndogo au mfadhili mwenye "interest" na Taasisi husika. Two sided argument kwenye kubadili mtazamo ni nzuri endapo mfadhili anaefuatwa ana kiwango kikubwa cha elimu, mwenye kutafakari, au hana taarifa juu ya Taasisi husika/ana mtazamo hasi juu ya Taasisi husika.
  3. Taswira ya Wanufaika (Potrayal of Beneficiaries). Wanufaika ni walengwa wa mradi, wanaweza kuwa watoto yatima, watu wasio jiweza n.k . Ili kubadili mtazamo wa mfadhili, Taasisi inapaswa kuwaonyesha wanufaika katika hali ya dhiki wanayopitia ili kujenga hisia za huruma kwa mfadhili. Japo wakati mwingine kuwaonyesha wanufaika katika hali hii huweza kutafsirika kama udhalilishaji , hivyo kukwaza baadhi ya wafadhili. Na ili kukabiliana na hili; baadhi ya wafadhili hawapendelei utajaji wa majina ya wanufaika au uonyeshaji wa sura za wanufaika. Hivyo kwenye jambo hili, ni vyema kujua mtazamo wa mfadhili mapema na utaratibu wake.

OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…