Kumuacha mkeo/mmeo na kuoa mchepuko, hiyo ni akili ya kawaida?

Kumuacha mkeo/mmeo na kuoa mchepuko, hiyo ni akili ya kawaida?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Inakuwaje pale uko kwenye ndoa yako ya miaka kadhaa huku mkiwa na watoto, baadaye inatokea ugomvi mnaamua kuachana na mke/mme wako mliyepambana naye kwenye shida mpaka hapo ulipofikia kwenye hatua fulani ya kiuchumi, na kuamua kuishi na mwanamke/mwanaume mwingine aliyekuwa mchepuko wako huko nyuma.

Je, hiyo ni akili ya kawaida?
 
Sioni tatizo hapo maana mshaamua kuachana sasa kuna ulazima gani wa kulazimisha kuishi pamoja hali ya kuwa hakuna maelewano tena, mwishowe mje muuane bure

Mkishindwa kuelewana ni vema kila mtu a move on ili kila mtu afurahie kile anachoona ni sahihi kwake
Mkuu,nadhani kuachana ni mchakato mrefu....mbaya zaidi kinachokufanya utengane naye ni ile hali ya kumchukia tu,na hakuna sababu nyingine.
 
Back
Top Bottom