Kumwanzishia mtoto chakula

KELLYN

Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
25
Reaction score
5
Je naweza kuanza kumpa mtoto wa miezi mitatu na wiki mbili juice za matunda? Uji au mtori na anatumia maziwa ya ngombe, ya kopo aliyakataa huwa nakwenda kazini nachelewa kurudi.
 
Kellyn

Mtoto wa miezi 3 bado hajafikia muda wa kuanza kula chakula, anatakiwa afikishe miezi sita ndio umpatie chakula. Maziwa ya mama yanavirutubisho tosha kabisa kwa mtoto, ingawa wengine wana lalamika maziwa hayatoshi na mtoto ananyonya sana, mpatie hayo hayo hatakama hayatoshi.
Hii itamsaidia mtoto

1. asiugue ugue kwani atakuwa amepata kinga ya kutosha kutoka kwa mama
2. anakuwa na akili yaani anakuwa bright darasani

Tafadhali temebelea kitua cha afya kwa maelezo zaidi
 
KELLYN

Kwanza kabisa maziwa ya ng'ombe kwa mtoto wa umri chini ya mwaka (miezi 12) sio mazuri.

Hawawezi kuya-digest vizuri na yana protein + madini kwa kiwango kikubwa zaidi ya ambacho mtoto wa umri kama wako anahitaji. Kwahiyo badala ya kumsaidia unampa uwezekano wa kupata matatizo.

Uji+mtori pia sio healthy kwa mtoto wa umri chini ya miezi sita. Ndio maana kuna watoto wanashindiliwa mavyakula lakini hawana afya kama wanaonyonya. Muhimu ni wewe mama kula vizuri (sio kula sana bali kula vyakula vya kila aina + matunda kwa kiasi cha kutosha) ili mtoto apate virutubisho. Ukila vizuri maziwa yatakuwepo (kama tatizo ni kuwa hauna maziwa).

Kama formula amekataa na wewe huwezi kumnyonyesha labda kwasababu ya kazi mkamulie maziwa yako awe anapewa ukiwa haupo. Jitahidi mwanao aishi kwa maziwa yako kwa kiasi kikubwa sasa hivi na sio maziwa yako yaishie kuwa supplimemt (kitu cha ziada/nyongeza). Hiyo ni kwa faida ya mtoto wako. Atakua vizuri kiakili na kiafya pia.

Jitahidi bana.
 
Last edited by a moderator:
Sina mtoto lakini nmefundishwa kuwa maziwa ya kila mnyama ni kwaajili ya mnyama wa aina ile, maziwa ya ng'ombe ni kwaajili ya mtoto wa ng'ombe.
Kitu kingine ni kwamba tunatofautiana kwa asilimia kubwa binadam na ng'ombe katika ukomavu wa ubongo.
Mtoto wa ng'ombe huzaliwa na ubongo ulio komaa kwa zaidi ya 90% ndio maana ndama huchukua mda mfupi tu na kuanza kucheza mwenyewe.

Mtoto wa binadam ubongo wake huwa bado hauja komaa kabisaaaa almost below 25% kama sikosei, kwa hiyo, ubongo wa mtoto wa binadam huendelea kukomaa kadri anavyo endelea kukua, na hii prosesi hufanyika ndani ya miezi kadhaa ya mwanzo, na prosesi hii husaidiwa zaidi na chakula cha mama (maziwa ya mama).
Help your baby to grow well dont give him/her cows milk so early, do it after six month it will be better.

Watu wengi ambao hawashindi nyumbani na watoto wao, hukamua maziwa yao (maziwa ya mama) na kuyaacha ili mtoto akihitaji maziwa anapewa.

I wish your baby a good health.
 
Zingatia exclussive breastfeeding kwa miezi sita kabla hujaanza mpa chochote, ina advantage kwako na kwa mtoto.

Kwanza utaongeza upendo na mwanao kwa kuwa nae muda mwingi, pili atapata nutrients zinazohitajika kwa wakati mwafaka kubwa kwa mama atapata natural contraceptive kwa miezi sita kama atamnyonyesha mwanae effective.
 
ahsanten kwa ushauri nitaufanyia kazi nampenda sana mtoto wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…