Kumwuliza maswali Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu; Aibu waandishi wa habari kugeuka Wabunge

Kumwuliza maswali Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu; Aibu waandishi wa habari kugeuka Wabunge

nicholasmari

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
630
Reaction score
583
Leo nimeona kioja baada ya Mkurugenzi wa Mipango ya miundombinu kuulizwa maswali na waandishi wa habari Dodoma kuhusu ujenzi wa miundo mbinu ya barabara. Hii ni kutokana na ufinyu wa uelewa wa waandishi wetu wa habari.

Waandishi wa habari walitakiwa kuuliza maswali ya kisera yanayogusa nchi nzima siyo specific qns kwa barabara zilizoko ktk maeneo husika.

Hayo maswali specific wameshauliza wabunge wa maeneo husika. Nyie mmetumwa na nani kuuliza hayo maswali?

Hata hivyo mkurugenzi ni mtu mdogo sana kujibu hayo maswali, hata mtendaji mkuu wa TanRoads hawezi kujibu, hayo ni maswali ya Waziri wa Ujenzi.
 
Back
Top Bottom