Uchaguzi 2020 Kuna alichojifunza mzee baba hadi sasa?

Mkuu sasa kama mnajua hivyo si mmwambie Lisu hizo hela bora akanunue kashamba kuliko kuhangaikia kitu ambacho hakipo?

Hapo mnaonyeshwa tu kuwa nchi hii haiwezi kuwa ya chama kimoja kwa ridhaa ya wananchi walio wengi. Bila kampeni mtaahadaa umma kuwa ccm na Magufuli wanakubalika sana.

Kampeni hizi zimekuja kuonyesha kuwa wanaoikubali ccm ndio hao hao, na wanaoukubali upinzani wapo tele. Kwahiyo mwambieni jiwe kuteka, kuua, na kulazimisha kuongoza watu kwa mitazamo yake ya kikomunisti, zana hizo zilishapitwa na wakati.
 
Ni wananchi ndio ambao ni wafuasi wa chadema,

Hata wananchi wafuasi wa ccm wamaweza kuimba hivyo kumwambia Lisu au Mbowe sasa hapo cha ajabu ni kipi?

Kabla ya kampeni hizi mlikuwa mnahadaa umma kuwa upinzani umekufa, lakini kupitia kampeni hizi, imefahamika kabisa kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki, ndio maana kinategemea hila kubaki madarakani.
 
Kura yangu haienddi kwa magu hatakidogo . Na machungu mengi mengi ukiachana na ajira Bab angu kastaafu mpaka leo hela hamna wakati ni haki yake

Hauko peke yako. Binafsi na jamaa zangu wengi tu tunausongo naye sana.

Haki na uhuru wetu hauwezi kuwa wa kuchezea chezea.

Maisha ya watu wengine kutokuwa issue kwake halisameheki hivi hivi. Leo ni kwa hao waliopotea kesho atafuata nani?

Hajatupa majibu nani walitaka kumwua Lissu na kwa nini. Wako wapi Sanane, Azory na wengine?

Kwa nini asituache sisi kuwachagua tuwatakao?

Mahakama, polisi, na mamlaka zote za serikali zikiwamo tume za uchaguzi zimejikita kwenye kumkandamiza mwananchi. Hii haukubaliki.

Hivi hasara inayosababishwa kwa hawa:

Kabla ya Lissu, Waziri wa Ujenzi atembelea barabara ya Rusahunga - Rusumo

serikali inawafidia vipi?
 
Kura yangu haienddi kwa magu hatakidogo . Na machungu mengi mengi ukiachana na ajira Bab angu kastaafu mpaka leo hela hamna wakati ni haki yake
Ukizingatia mzee baba ulishaweka mipango yako kwenye fungu la mzee
 
Aongezewe miaka mingine ya ushamba na ulimbukeni wa kutupa ,hivi kweli usiongeze mishahara miaka mitano , usipandishe madaraja miaka mitano , watu watekwe wauwawe , udhulumu wastaafu , ule hela za wahanga wa tetemeko la kagera na hela za korosho ? Watu wakuchague hiyo itakuwa akili matope ?
 
Sasa na watu wengine wakifanya maandamano kama hayo ku support magufuli au kumsema Anti , ndio itakuwa ndio msimamo wa majprity of Tanzanians ?
Wewe jamaa vipi aise mbona unauliza swali Kama mtoto.

CCM fanyeni tu ndo Haki yenyewe MH TL anawapigania hiyo.

Ila hamjielewi ni kama zombies tu!
 
Leo kasema wamuonee huruma
 
Ni mtu wa ajabu sana. Yaani utadhani ni jitu fulani hivi halina akili.
 
Leo kasema wamuonee huruma

Ni vizuri akatambua kuwa hapendwi. Hakuna maneno mazuri ya kumwelezea zaidi ya hilo.

Kulitambua hilo na kulifanyia kazi ndiyo ilikuwa uungwana.

Abadilike. Watanzania ni wenye kusamehe.
 
Na wako wanaoshabikia kuenezwa kwa chuki hizo kana kwamba madhara yake yanakomea kwa jirani

Hao ni wale wanufaika wa moja kwa na mzee baba. Hao hata ikiwa kupokea bakora asubuhi na jioni hawawezi kuachana na mapambio ya kusifu.

Humo wamo wateule, kina ndugayi ndugai, watarajia teuzi kama kina manjaa manjaa na lile kundi pendwa lb7 ambalo maugonjwa matambuka ni member wake makini zaidi akifuatiwa na ngedere wa 'ikungu lya bashashi'.
 
Wewe jamaa vipi aise mbona unauliza swali Kama mtoto.

CCM fanyeni tu ndo Haki yenyewe MH TL anawapigania hiyo.

Ila hamjielewi ni kama zombies tu!
U ought 2 be a stupid of a highest order , by thinking that what U want U will get it throught maanamb787
 
Kura yangu haienddi kwa magu hatakidogo . Na machungu mengi mengi ukiachana na ajira Bab angu kastaafu mpaka leo hela hamna wakati ni haki yake


Tulia dogo, ela ya Baba yako ndio inajengea bwawa la umeme na SGR.

Wewe na Baba yako hampendi maendeleo ya vitu???
 
Mkuu!

Acheni kushinda mitandaoni njooni huku mitaani jamani huku ndio kura zilipo.

Yani kwa jinsi hali ilivyo huku ni kama vile watu walishajitayarisha kumpitisha Magu.

Sioni upinznai mtatokea wapi mwaka huu
Unadhani sisi tunalea mapacha wa maria tupo field magufuli out hata suku.ma land imemyema
 
Kosa la CCM ni kumkumbatia Magufuli. Kuna maovu ya kutisha ambayo Magufuli ameyafanya ambayo hakutumwa na CCM na wala siyo ilani ya CCM.

CCM haikumtuma Magufuli;

  • Kuteka watu
  • Kuuwa watu
  • Kupiga watu risasi
  • Kudukua mawasiliano ya watu
  • Kutoongeza wafanyakazi mishahara
  • Kuua biashara
  • Kuweka watu ndani kwa makosa ya uongo
Sasa kwakuwa CCM imemkumbatia muovu, kipigo ni kwa CCM na huyu nduli
 
Jamaa kama ni timamu kichwan atakuwa kapata somo kubwa Sana.... Kuwa upinzani upo upo Tena na hasira juu
 
Kampeni za ccm ni kama fiesta tu watu wanakwenda kuangalia wasanii mziki ukiisha wanamuacha Meko anapayuka peke yake

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…