Kaka,
Mimi nimeshawahi kununua Alibaba vitu tofauti tofauti, mara kadhaa kwa muda sasa.
Kuna wafanya biashara wazuri Alibaba na pia kuna matapeli kama ulivyosema. Cha msingi ni kuwa makini na mtu unaefanya nae biashara. Angalia kama ni "Gold Supplier" na kama amekuwa "Verified" na Alibaba. Hizi ni moja ya hatua za awali kuhakikisha kama haufanyi biashara na tapeli.
Make sure you transact with a verified supplier.
Pili, cheki kama wana website, na itembelee website yao. Wafanya biashara wengi wa China walio makini wanakua na website nzuri kuonyesha umakini wao.
Pia, mwambie akupe physical address yake na mtaarifu kuwa una mtu China ambae atakuja kufanya local pick-up. Wafanya biashara wengi matapeli utawajua tu inapofikia hatua hii.
Kama bado unasita, nitumie link ya Alibaba profile ya hiyo kampuni unayotaka kufanya nayo kazi nione kama naweza kukusaidia.
Mimi nimenunua vitu Alibaba mara nyingi. Na hata last month nimepokea mizigo miwili kupitia EMS na DHL. Sijawahi kutapeliwa, ila inahitaji uwe makini sana. Wachina ni tapeli sana.