Duh!! hii kali sasa.....Sikonge, Mwafrika, na Rev. Masanilo hebu tuwekeeni zile picha za maisha bora kwa kila Mtanzania....e.g. zile za wale madogo waliokaa chini darasani au zile za akina mama wajawazito na wale walijifungua kulala sakafuni.....
Kwa ufahamu wangu, asilimia kubwa ya watz wanaishi vijijini, ambako shughuli nyingi za maendeleo yao zinapita kwenye kamati za maendeleo za maeneo hawa angefuta utaratibu wasingekumbana na kadhia hizo.
Picha za kinamama waliolundikana kwenye wodi za uzazi, zimetoka DSM, ambako wengi amehamia jijini humo pasipo sababu za msingi. Hii haijalishi usalama wao wa kujifungua katika mazingira muafaka. Tatizo hapa ni kuzidiwa kwa vituo vya afya kutokana na uhamiaji wa watu hao.
Nchi yetu inajengwa na kata, tarafa, wilaya na mkoa. Iwapo wilaya ama kata inakuwa na tatizo fulani, mwenye jukumu la kuondoa tatizo hilo ni wale ambao wanaishi kwenye eneo hilo. Iwapo wao binafsi kulundikana kwenye hospitali sio tatizo kwao, hata ije serikali yoyote ile tabia ya kulundikana haitoweza kubadilika.
Maendeleo ya wananchi yatatokana na kero ambazo wanaziona, kupita kamati zao wanauwezo mkubwa wa kuondoa kero hizo. Matatizo makubwa miongioni mwa wananchi ni ujenzi holela(hii ni kutokana na uhamiaji holela), taka ngumu na taka maji, shule, zahanati, n.k
Iwapo katika level ya kata wataweza kujua kero zao, hapana shaka kutakuwepo na unafuu mkubwa katika ngazi ya wilaya na mkoa vilevile.
Wakati wa kusubiri kupangiwa kila kitu na serikali kuu umepita, ni jukumu la wananchi kujipangia vitu wanavyotaka katika maeneo yao, ili kuboresha maisha yao ya kila siku.