Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu salam,
Kesi ya watuhumiwa wa kesi ya Yombo imeanza kuunguruma Jumatattu baada ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani. Kimtaani mtaani tunajua kilichowapeleka pale ni kumlawiti na kumbaka binti yule.
Mpaka sasa sijakutana na hati ya mashtaka ya watuhumiwa hao, na hata katika kuuliza kwa watu wa karibu ikiwemo wanasheria nao hola!
Pia soma: Yaliyojiri kesi ya Binti wa Yombo Agost 20, 2024: Shahidi mmoja asikilizwa, Watuhumiwa wamerejeshwa rumande
Kwanini document hii haijawekwa wazi? Mpaka sasa polisi hawajatoa taarifa hii, tunapata ripoti kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya habari. Kwanini hatupewi taarifa rasmi?
Hii inaonesha fika jinsi jeshi la polisi lilivyokuwa na maslahi katika kesi hii. Tunataka uwajibikaji na hili linajumuisha pia kujua hawa wanyama wanawajabika kwa udhalimu, hii ni pamoja pia na kuwa na taarifa sahihi ili kuweka rekodi sawa.
Polisi na wahusika wote tunajua mnapita humu, wananchi tunataka hati ya mashtaka tujihakikishie uso kwa macho.