Kuna baadhi ya maneno yakitumika kunogesha soka, kwa wengine si "sanaa" bali huleta maumivu

Kuna baadhi ya maneno yakitumika kunogesha soka, kwa wengine si "sanaa" bali huleta maumivu

babacollins

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
901
Reaction score
212
"Sanaa ya Uandishi" ni neno nililolisikia siku chache zilizopita baada ya tukio la kupigwa mashabiki kiwanjani walipoenda kwa kusudi la kutazama mchezo wa soka.

Baadaye kilichofuatia ni tamko kutoka katika uongozi wa Simba. Lugha iliyotumika kukemea tukio la kupigwa mashabiki hao ndio iliyofikia hapo kwenye sanaa ya uandishi na kuzua maswali mengi na mjadala kwenye vyombo vya habari.

Lakini kwenye mchezo wa soka imekua ni kawaida sana kwenye baadhi ya vyombo vya habari kusikia lugha ambayo kitaaluma sidhani kama ni busara kuitumia. Nimeshawahi kusoma na kusikia timu "...imepigwa na kitu kizito..." au "...kitu chenye ncha kali..." kwa maana ya kufungwa.

Maneno haya ni rahisi sana kuyatamka na kuonekana kama yananogesha lakini mara nyingi tunapoyasoma au kuyasikia katika maswala mengine yasiyo ya kimichezo yanaambatana na mtu/binadamu kupoteza uhai.

Kwa waliofikwa na madhila ya namna hiyo kuyasikia au kusoma maneno hayo katika namna inayokusudiwa michezoni haswa soka ni jambo la kusononesha mnoo. Kwao sio jambo la "sanaa" au kufurahisha hata kidogo.

Ni mimi mchezaji kiongozi.
 
Back
Top Bottom