Kuna bomu linakaribia kulipuka muda wowote

Sahihi kabisa
*"""Haiingii akilini mtu anasoma muhimbili five years halafu AA anakuja kuwa bodaboda au kuuza kahawa mtaani. Kuuza kahawa hakuhitaji degree wala masters"""
 
Hapo ndipo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inapolaumiwa walimu mia 200 wanazurura wakati shule za Sekondari hazina walimu wa kutosha?
Uko wapi nikuletee walimu 200 wanaozurura mtaani sasa hivi mwaka wa 3 ukawape ajira kwenye hizo shule za kata?
 
Anajitoa ufahamu huyo, wakati jiwe ndie aliyeongeza ukosefu wa ajira kushindwa kuajiri wahitimu wa vyuo vikuu huku akijificha nyuma ya wamachinga na boda na kuwafanya wafanye shughuli zao popote pale baada ya kushindwa kutoa ajira.
 
Shida kubwa ilisababishwa na Magufuli alisimamisha kila kitu, kwenye UALIMU ndio aliharibu kabisa mtu unaanza na TGTS D1 kama ni degree ambayo ni 716.000 unafuu ulikuwa kupanda daraja yeye akaongeza miaka ya kupanda daraja kutoka minne kwenda mitano. HAKUWA KABISA NA UBINADAMU.
 
Njoo mkoa wa Mwanza wilaya ya Kwimba kata ya Maligisu kuna shule mpya hapa Maligisu Center ina walimu 2 tuuu.

Acheni kukaa ofisini tembeeni muone maajabu
 
Mkuu Tanzania Kuna ajira nyingi sema wenye ajira ndo wanapewa ajira tena mfano mdogo tu TASAf ina fursa kibao ila hizo fursa wanapewa walimu na baadhi ya watendaji wa kata happy wasiokuwa na kitu wangepewa Kama part time kwao tungepunguza rate ya hao uneployment
 
Najua humu kuna watu wa level tofauti za elimu na uwezo tofauti wa kupambanua mambo binafsi nawaomba kwenye hoja ya population muiache kabisa hasa katika muktadha mnaozungumzia, mnaweza mkamlaumu mwendazake kwa mambo mengi sana ila kama kweli akili zenu zinafanya kazi vizuri basi mtaona na mazuri mengi aliyoyafanya katika taifa hili, kwanza kabisa suala la unemployment katika mataifa mengi ya kiafrica hayasababishwi na high rate of population growth sababu mataifa mengi ya kiafrika yana idadi ya watu ambayo ni ndogo ukilinganisha na rasilimali iliyopo bado tunatakiwa tuendelee kuzaliana kwa wingi angalau kumeet lile gap la rasilimali na population tuliyonayo.

Ukosefu wa ajira ni matokeo ya mifumo mibaya ya kielimu ambayo inamsaidia kijana kuondokana na ujinga tu na sio kuwa innovative katika mazingira yake hilo ni pamoja na sera mbaya katika kusimamia mgawanyo sawa wa rasilimali zinazopatika katika maeneo yetu. Kwa upande mwingine chukulia mfano babu zetu hawakuwa na ajira na walikuwa na wake wengi na watoto lundo na waliwasomesha wote waliokuwa tayari kwenda shule just kwa shughuli za kilimo na ufugaji leo sisi vijana tumesoma wote tumekuja daslam tumelundamana hapa tumeacha vijijini kwetu maeneo makubwa yamekuwa mapori maana hakuna shughuli za uchumi zinazoendelea huko wote tunataka kukaa ofisini kwa kifupi tumekuwa WAVIVU sana hatutaki tena kazi ngumu tuko tayari kuwa wapambe wa watu waliofanikiwa bila aibu tumeuza UTU wetu na wengine wameenda mbali zaidi wameuza jinsia zao kwa wanaume wenzao ili tu aweze kuishi mjini.

Tujitafakari sana kama taifa maana wazungu wametuingiza kwenye mtego wa mda mrefu na sasa tumenasa maana walituletea elimu ambayo ilitakiwa ituwezeshe kutumwa na wao na sasa tumekuwa watumwa wa kifikra.
 
*"""Haiingii akilini mtu anasoma muhimbili five years halafu AA anakuja kuwa bodaboda au kuuza kahawa mtaani. Kuuza kahawa hakuhitaji degree wala masters"""
Hebu tupe mfano au jina la daktari mmoja dereva wa bodaboda au muuza kahawa.
 
Nenda pale posta katikati Kuna jamaa anaendesha bodaboda anaitwa sareh juma anatoka kigamboni. Amemaliza muhimbili MD lakini anaendesha boda
Una hakika amefaulu? Siyo hoja kupiga miaka mitano Muhimbili. Au vyeti feki lakini cheti cha MD cha uhakika hakuna dereva bodaboda wala muuza kahawa mtaani. Anaweza kukaa mwaka mmoja au miwili lakini kazi anapata hata kwenye private hospital.

Sizungumzii vyeti vya ualimu au sociologists
 
Mi nazungumzia MD siyo walimu. Hata hapa mtaani mjimwema wapo ma MD kibao kipindi Cha jk ndo ulikuwa huwezi kumkuta MD mtaani Hana ajaira
 
Kama ni halikulipuka kipindi kile ambacho ajira 0 zilikuwa zikitolewa na serikali lije lilipuke muda huu?
 
Our education system is irrelevant to the current situation......serekali itaajiri wangapi?

Inatakiwa ikidhi mahitaji yaliyopo. Kwa mfano aliotolea wa mwalimu wa physics kufundisha form one hadi four. Na kuna shule hazina sayansi sababu ni walimu tu.

Serikali inawajibu kuhakikisha sehemu zote za uhitaji wa wafanyakazi iajiri.

Wakimaliza hakuna atakaye ilaumu, tutaangalia ni namna gani inaweka mazingira ya uwekezaji.

Ikiwa kama mwajiri mkuu, ni lazima itatue tatizo la ajira.
 
Wapo mkuu tena kuna mwamba nauza nae mitumba ni md kahitimu Bugando, na intern kapiga Benjamin Mkapa!

Anafurahia kuitwa dokta, hana kitu.


Nimepiga nae stori kasema, wangi wameamua kujitolea kwenye hospitali binafsi kwa malipo ya pungufu ya 500k na mbususu za manesi.

Hata Bugando wanaozidi malipo ya 1m kama md ni wachache, tena na kamisheni ya bima ikiwemo.

Hali ni tete, na wenye mamlaka wanajua.

Maco na manesi hata hawana idadi mtaani, na miaka 10 kutakuwa na wapaka kucha ma_co.
 
Hii nchi imeharibiwa baada ya siasa kupewa kipaumbele na hivyo kuwafanya wanasiasa kuwa na nguvu na hivyo kutaka kufanya kila jambo kisiasa siasa, na hii ni toka enzi za mwalimu.........matatizo yote yanayoikumba nchi ni kutokana na mfumo wa hovyo wa kisiasa.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…