Kuna bomu linakaribia kulipuka muda wowote

Bibi alishasema kuwa siyo kazi ya serikali kutengeneza ajira!!
 
Mkuu awamu ya 5 tulifungua viwanda vipya 5,000+! Hawa wasomi kwanini wasiajiriwe mle?
 

Vijiwe vya kahawa, boda Boda na Vijiwe vyengine mitaani wanamtukuza sana mwendazake.
 
Ajira zenyewe zilizobaki ni bodaboda
Boda boda zinatengenezwa China, bajaji zinatengenezwa India. Sisi tuliua viwanda vyetu vya kutengeneza badkeli, nguo, mwatex, mutex, vya kusindika kahawa, vya kutengeneza betri, matairi, n.k.

Vijana wanaenda kusoma mechanical engineering ili wafanye kazi viwanda vipi?

Nyerere alivyoanzisha vile viwanda na Magufuli alivyokuwa akihimiza uanzishwaji wa viwanda walikuwa na maana yao. Haya mapoyoyo yaliyo hai hayana vision hata kidogo.
 
Lakini SI wiki umepitia tu tangu wameanza kulalamika humu na kwenye vipaza sauti kuwa Kuna ajira kubwa sana ya Waendesha bodaboda!
Pale tu Muona maono LEMA aliposema tu ni Jana na Laana!!

Ama kweli CCM ni mchwa hatutaacha kuona mengi!
 

..Magufuli alihimiza viwanda huku akitumia mabilioni kununua midege toka kwa mabeberu.

..badala ya kununua ndege alipaswa kujenga viwanda.

..pia akatumia mabilioni mengine kujenga mji wa Dodoma kwa ajili ya viongozi wa serikali.

..maana yake Magufuli alikuwa na fedha za kujenga mji wa viwanda badala yake akajenga mji wa serikali na wanasiasa
 
Nakazia hapa
Ni kweli serikali haina uwezo wa kuajiri haya majitu yote lakini hata kuichallenge serikali hayawezi?
Yamepata elimu na elimu haijayasaidia chochote kupata elimu siyo kwaajili ya ajira tu, tunategemea jamii yenye wasomi iende Kisomi tuone wasomi wakibadilisha jamii kupitia changamoto mbalimbali kwenye jamii zetu moja wapo ndiyo siasa za nchi hii zilivyo
Mambo yanavyoenda nchi ni kama hakuna walioelimika vile
 
Yaani ukijitoa muhanga, hutopata 1000 tu, maana vijana wengi mtaani wamekata tamaa, wako tayari kwa lolote, sema wanakosa wa kulianzisha tu..
Tatizo silaha mkuuu tukipata AK 72 kama buku basi tunaweza
 
Jamaa kaandika kile anachokiona wewe unakuja kumuuliza swali. Kwanza hakuna serikali duniani inaweza kuajiri watu wake wote iwe ajira za muda mrefu au mfupi. Inachofanya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kujiajiri au kutengeneza ajira za muda mfupi ikiwa ajiri za muda mrefu hazipo, hii itasaidia vijana kupata mitaji ya kujiajiri.
 
Inachofanya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kujiajiri au kutengeneza ajira za muda mfupi ikiwa ajiri za muda mrefu hazipo, hii itasaidia vijana kupata mitaji ya kujiajiri.
Upo sahihi Serikali unafanya hivyo kweli Ila still bado vikwazo ni vingi, mitaji kwa mshahara wa 100,000 kiwandani wakati Chuo ulisoma kozi unalipa M3 kwa mwaka hapo hujaweka gharama zingine does it make sense?
 
Mkuu hujanielewa labda kwasbb ya lugha, ni limaanisha mfumo wetu wa elimu hauendani na hili halisi ya sasa, unategeneza wasaka ajira sio wategeneza ajira
Joyce Ndalichako ndio Waziri mwenye dhamana mboni sijamsikia akilizungumzia hili?, sana sana nimeona mama saa100 analisemea vijana wajiajiri, mfumo huu wa elimu umesimamiwa na Ndalichako kwa kipindi kirefu na sasa yeye ndie Waziri mhusika masuala ya Ajira Vijana wako uliowasimamia kipindi wewe ni Waziri wa elimu wamesoma wamemaliza sasa wengi wamezagaa mtaani hawana Ajira hawana kazi angalia namna ya kuwatafutia angle mama mtaani kunachosha,
 
Lakin mtu mwenye master kweli analalamika ajira au anachagua kazi mkuu? Sasa sisi wa la saba tufanyeje. Mi siamini aisee.
 
Bado tu kuna unemployment nchi hii?

Si tunaambiwa kwa sasa mambo ni safi ajira zinatangazwa mara mbili hakuna waombaji?

BTW:Nimeona taarifa ongezeko la vijana wanaoenda kwenye hospital nchini kuulizia kama wanaweza uza figo zao pale.
 
Sehemu zinzazofaa Kwa kilimo zinaainishwa vijana wazame shambani ushamba Sasa nidili
 
Waitoe CCM madarakani wakiweke chama gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…