Mondoros
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 629
- 474
Baba wa Taifa la Sangapore LeeKuan Yew aliposhinda uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza mwaka 1959 alikuta nchi ipo katika hali mbaya sana katika huduma za Afya,Elimu,Rushwa na ufisadi,ajira,viwanda,miundombinu,umaskini uliokubuhu n.k. Alipoingia madarakani bwana Lee alikuwa na kazi moja tu ya kujenga Singapore mpya yenye uchumi uliobora,huduma za jamii zilizobora pamoja na miundombinu mingine inayohitajika kwa maslahi ya taifa.
Bwana Lee alitumia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha anasimamia serikali itakayowanufaisha wanyonge bila ya kuwaathiri matajiri huku akiongozwa na kauli ya “binadamu hawapo sawa” baadhi ya mbinu alizozitumia toka mwaka 1959 mpaka 1961 ni-:
1. Alifuta haki za binadamu kwenye katiba ya Singapore
2. Aliwaondoa wafanyakazi wote wasiokuwa waaminifu(wala rushwa) katika serikali yake na kuwapa kazi vijana wasiokuwa na uzoefu wowote na shughuli za serikali
3. Aliwafungulia mashtaka mafisadi wote nchini Singarepore na wote walipatwa na hatia walinyongwa hadharani
4. Mtu yeyote aliyekuwa anapinga au kukejeri jitihada za serikali hadharani alikamatwa na kupelekwa gerezani
5. Alihamasisha watu kufanya kazi kwa nguvu zote huku serikali yake ikitengeneza mazingira bora ya wananchi kufanya kazi
6. Alitengeneza mazingira bora ya uwekezaji na kuweka sera bora na sheria rahisi za kuwekeza Singapore na alitafuta wawekezaji ndani na nje ya nchi yake kuja kuwekeza nchini mwake
7. Alismiamia nidhamu ya watumishi wa serikali na wananchi
Katika kipindi hicho cha miaka 2 ambayo bwana Lee alikuwa anajenga mfumo mpya wa nchi ya Singapore yalitokea mambo mengi sana magumu ikiwemo ajira kushuka kwa kiasi kikubwa,baadhi ya viwanda kufungwa,huduma za jamii kuzorota ikiwa ni pamoja na huduma za afya,maji,elimu n.k. Mbali na magumu hayo yaliyoikumba nchi ndani ya kipindi kifupi ila wananchi wa Singapore bado waliendelea kuwa na imani kubwa na bwana Lee kutokana na jitihada zake za kupambana na rushwa,kubana matumizi,kuleta nidhamu serikalini,kuboresha miundombini ya umeme,barabara,reli na viwanja vya ndege n.k
Kwasasa nchi ya Singapore ipo katika nchi za dunia ya kwanza(first world country) toka nchi ya dunia ya tatu(third world contry)…….
Lee Kuan Yew aliongoza kama waziri mkuu wan chi hiyo kwa miongo mitatu mfululizo na alijiuzuru nafasi hiyo mwaka 1990 ila aliendelea kuwa kuhudumu katika serikali kama waziri na mbunge mpaka pale mauti yalipomfika mwaka 2015.
by
Ogulu