Kuna dawa ya kupunguza Kukohoa?

Esrom makono

Senior Member
Joined
May 11, 2019
Posts
121
Reaction score
76
Samahan waungwana Nina tatizo kurekebisha koo/kukohoa kwa kuhisi Kama nna kikohoo lakin sivyo.nimepima afya iko njema kifua Safi nikapewa dawa ikatulia kidogo lakin Tena Hali imejirudia.shida itakua nn? Je Kuna dawa naweza tumia hata asili nikaepukana na hii Hali?
 
Tumia tangawizi, pilipili manga, mdarasini, asali, aina ya viungo jamii hiyo huwe unameza kijiko jinsi unavyijisikia kikoozi kwishne
 
Lakini hapo kwenye matumizi navitumiaje? Nachanganya vyote au??
 
Mazingira yako ya hewa yakoje! Je ni vumbi sana, mkaa ama vipi? Epuka kuishi na hewa chafu
 
Nafuna vitunguu maji Kwa siku kimoja... Muda wa siku 5
 
Jaribu kutumia asali ila iwe original maana siku hizi fake kibao.
 
Hizo dawa zote mlizotaja hazitaweza kumsaidia bila kwenda kwa specialist.
Anaonekana ana tatizo la alergy na kitu fulani either vumbi au kitu kingine kinachofanana na hicho.
Kama si hivyo Basi ana kikohozi kikavu ambacho kwa dawa za kawaida haziwezi kusaidia.
 
Dah pole sana
 
Umeangalia "kilimi?

Umebadili manukato, sabuni au mafuta ya kujipaka?

Je umepaka rangi fanicha au nyumba unayoishi?

Umepima Minyoo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…