Dawa hizo za vidonge ziko kwenye maduka mengi ya madawa. Ukienda famasi ukasema unahitaji vidonge vya fansida aina ya "ROCHE" ambalo ndilo jina na brand ya dawa hiyo, basi muuzaji atakuletea hayo mavidonge fake ambayo hata brand yake ni tofauti kabisa na Roche yenyewe Brand yake ni ALKADER.Hata kwenye website ya roche dawa nyingi za zamani na mpya zimeorodheshwa ila hayo mavidonge fake hayamo na wala hawayatambui. Jamani naomba msaada, ni wapi ntapata vidonge original vya ROCHE?