Kuna dawa za vidonge fake zimeingizwa madukani zinaitwa alkader

CHETTA

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
27
Reaction score
3
Dawa hizo za vidonge ziko kwenye maduka mengi ya madawa. Ukienda famasi ukasema unahitaji vidonge vya fansida aina ya "ROCHE" ambalo ndilo jina na brand ya dawa hiyo, basi muuzaji atakuletea hayo mavidonge fake ambayo hata brand yake ni tofauti kabisa na Roche yenyewe Brand yake ni ALKADER.Hata kwenye website ya roche dawa nyingi za zamani na mpya zimeorodheshwa ila hayo mavidonge fake hayamo na wala hawayatambui. Jamani naomba msaada, ni wapi ntapata vidonge original vya ROCHE?
 
Mkuu hizi habari Taasisi ya dawa na chakula TFDA wana taarifa..? Maana hili ni janga sasa kama kuna dawa fake kwenye maduka ya dawa..!
 


Mkuu,umetumia sababu gani kuita hizo dawa ni fake?Nijuavyo mimi ni kuwa hiyo dawa Fansidar inatengenezwa na manufacturers mbali mbali mmoja wao akiwepo huyo aliyotengeneza brand ya ROCHE

Pia hiyo brand ya ALKADER imetengenezwa na manufacturer mwingine akaiita hivyo..Lakini na yenyewe bado ni Fansidar na inatumika kumanage the same disease

Sasa inawezekana therapeutic efficiency ya brand mbili za dawa from two different manufactures ikatofautiana,lakini bado hii haiifanyi mojawapo kuwa fake

By the way,,kama una doubt zaidi jaribu kuwasiliana na TFDA ili kuepusha madhara kwa wengine
 
Ukigoogle Fansidar Roche inaipata na inaelezwa ni dawa ya kutibu au kuzuia malaria, lakini ukigoogle fansidar alkader hupati information yoyote. Nadhani uwezekano kwamba ni feki ni mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…